Thursday, February 7, 2013

53 WAFARIKI KWA AJALI soma zaidi

Watu wasiyopungua 53 wamefariki katika ajali ya basi kaskazini mwa mji mkuu wa Zambia Lusaka. 
 http://resources1.news.com.au/images/2013/02/08/1226573/104285-zambia-bus-crash.jpg
Imeripotiwa kuwa basi hilo liligongana na lori lililokuwa linatoka upande wa pili karibu na mji wa Chibombo. Watu wengine 22 wamejeruhiwa katika ajali hiyo. Basi hilo linalomilikwa na shirika la huduma za posta la Zambia, lilikuwa limebeba abiria kati ya mkoa wenye machimbo na  mji mkuu jana Alhamisi. Hilo ndiyo tukio baya zaidi kuikumba nchi hiyo katika miaka ya hivi karibuni. Takwimu rasmi zinaonyesha kuwa karibu watu 1200 wanauawa katika ajali za barabarani nchini Zambia kila mwaka.

No comments:

Post a Comment