Thursday, January 31, 2013

ASKARI POLISI NA MTUHUMIWA WA MAUWAJI YA MWANGOSI WAKIMBIA CHUMBA CHA MAHAKAMA ,HAKIMU AGEUKA MBOGO.


Hapa mtuhumiwa  huyo akikimbiziwa mahabusu ili kukwepa picha ya  wanahabari leo
Hapa akiingizwa mahakamani leo
                                        
Huyu ndie mtuhumiwa wa mauwaji ya Daudi Mwangosi

Na Francis Godwin
 
SAKATA la mtuhumiwa wa mauwaji ya  aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha Chanel Ten mkoani Iringa marehemu Daudi Mwangosi limezidi kuchukua  sura  mpya baada ya askari waliomfikisha mtuhumiwa  huyo wa mauaji  askari  wa FFU mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23) kumtibua hakimu na kuageza mtuhumiwa huyo kurudishwa tena kizimbani kwa kudharau mahakama hiyo.

Tukio  hilo lilitokea leo  majira ya saa5.35 kwa  askari  hao watatu ambao majina yao hayakuweza kufahamika mara moja  kumshusha  kizimbani mtuhumiwa  huyo wa mauwaji na kumkimbizia mahabusu kama njia ya kukwepa kupigwa picha na wanahabari  waliokuwepo hapo lilitokea mara baada ya mahakama hiyo kuombwa kutaja tarehe nyingine ya  kutajwa kesi hiyo.

Huku  bado mahakama ikiwa inaendelea kwa hakimu kutaja tarehe ya kesi hiyo namba  ya mauwaji kesi namba 1 ya mwaka 2012 mtuhumiwa wa mauwaji alishuka kizimbani  huku akivaa kofia yake ya sweta (mzula)na miwani ya giza na kuanza  kushuka jukwaani kabla ya hakimu kumtaka mtuhumiwa huyo kutovalia kofia hiyo kizimbani huku kabla ya mahakama  kumalizika.

Wakati hakimu  huyo akijiandaa kusimama ili kuhitimisha shughuli za kimahakama kwa siku  hiyo ghafla alijikuta anabaki na mwanasheria  wa mahakama ,kalani wake ,wanahabari ,askari mmoja na ndugu  wawili wa mtuhumiwa huyo  huku askari  watatu wenye silaha  na mtuhumiwa huyo  wakiwa tayari wameondoka ndani ya chumba cha mahakama hiyo.

“Mbona hao askari wanamtoa mtuhumiwa  bila utaratibu wa mahakama hebu  mwanasheria waambie wamrudishe ndani mtuhumiwa ....huu si utaratibu mbona  wanafanya fujo mahakamani  hao” alisikika akisemahakimu mkazi  wilaya ya Iringa Dyness Lyimo

Hata  hivyo pamoja na jitihada za mwanasheria   wa  serikali Adolf Maganda kuwaita  kwa  sauti  askari hao  kuwataka  kumrudisha  ndani ya mahakama mtuhumiwa huyo  bado askari  hao  walizidi kukimbia na mtuhumiwa kwenda nae mahabusu na baada ya dakika kama 5 hivi ndipo mwanasheria  huyo aliporejea na askari hao na mtuhumiwa ambae hata  hivyo hakwenda kusimama  kizimbani na badala  yake alikwenda upande wa  kushoto wa mahakama  hiyo ambako alikuwa amekaa mwanzoni kabla ya mahakama  kuanza na kuketi katika  kiti huku akiwa amevaa miwani na kofia  yake.

Kutokana na  tukio  hilo hakimu  huyo alilazimika  kuwahoji askari hao  watatu kwa vurugu  hizo  walizozifanya kwa kuwauliza swali moja  pekee  kuwa  wanaona walichofanya ni  sahihi na askari hao kuomba msahama  kuwa samahani mheshimiwa.

Mwendesha mashtaka  wa jamhuri Adolf Maganda aliiomba mahakama hiyo kutaja tarehe nyingine ya kutajwa tena  kesi hiyo ambayo ilitajwa Januari 27 na mtuhumiwa huyo kushindwa kufika kutokana na tatizo la ugonjwa  lililokuwa likimsumbua .


Hata  hivyo mahakamani  hiyo  liahirisha  kesi hiyo  hadi  Februari 14 mwaka huu kesi hiyo itakapofikishwa mahakani hapo kwa  kutajwa tena.

Mtuhumiwa  huyo anatuhumiwa  kumuua kwa    bomu aliyekuwa  mwandishi  wa habari wa Chanel Tena  mkoa  wa Iringa  marehemu Mwangosi  septemba 2 Septemba mwaka jana  katika kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa  wakati  wa vurugu kati ya  polisi na wafuasi wa  Chadema .kinyume na kifungu cha sheria namba 148 kifungu kidogo 5A.i cha makosa ya jinai. Kwa mujibu wa kesi za jinai, sheria kifungu 196 kanuni ya adhabu Cap. 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002

No comments:

Post a Comment