Zaidi ya shilingi milioni mbili na laki nne zimetumika
katika ukarabati wa baadhi ya majengo katika shule ya msingi Kisinga kata ya
Lupalilo wilayani Makete
Akizungumza ofisini kwake mwalimu mkuu wa shule ya msingi
Kisinga Bi. Tulumbe Kyando amesema kuwa ukarabati wa shule hiyo ni pamoja na
vyoo vya nyumba za waalimu, madarasa saba na ofisi mbili za waalimu
Amesema wakati wa ukarabati huo wananchi nao walikuwa
wakishiriki zoezi hilo
ambalo lilikuwa likifanyika siku za mwisho wa wiki Ijumaa na Jumapili
Mwalimu Kyando amesema fedha hizo zilizotumika kwa ajili ya
ukarabati hazikuchangwa na wananchi kama
ilivyozoeleka badala yake zimetokana na kuuzwa sehemu ya msitu wa shule hiyo,
ambapo fedha hizo zimetumika kununua saruji, mchanga, mbao pamoja na vioo
Mwalimu huyo amemshukuru afisa mtendaji wa kijiji hicho
pamoja na wananchi kwa kutoa ushirikiano kufanikisha ukarabati huo, kwani hiyo
ni njia mojawapo ya kuboresha elimu wilayani Makete
Katika hatua nyingine Afisa mtendaji wa kijiji cha Kisinga
Bw. Raphael Tweve amesema katika ukarabati huo waliweka mkakati wa kusogeza
maji shuleni hapo, mkakati ambao wameutekeleza
Amesema hapo awali kulikuwa na tatizo la shule hiyo kukosa
maji, lakini kwa hivi sasa tatizo hilo
litatoweka
No comments:
Post a Comment