Monday, November 19, 2012

WANYAMA WAHARIBIFU WA MAZAO WAIBUKA UTANZIWA WILAYANI MAKETE

Hawa ndo nyani wanao haribu mazao huko Utanzawa




Na Hadija Sanga
Kumeibuka wimbi la wanyama waharibifu katika kijiji cha Utanziwa kata ya Bulongwa wilayani Makete ambao wanaharibu mazao yaliyopo mashambani pamoja na mifugo ya wakazi hao
Akizungumza na wandishi wetu ofisini kwake, afisa mtendaji wa kijiji hicho Bw. Paulo Simon Chaula amesema kuwa kijiji hicho kinakabiliwa na wanyama waharibifu wa mazao ambapo kwa kiasi kikubwa wamesababisha hasara kwa wakazi hao
Amesema wanyama hao waharibifu wa mazao ni jamii ya nyani ambao wameanza uharibifu huo bila ya wao kujua walipotokea ambapo mpaka sasa bado wanaendelea na uharibifu huo
Amesema wao kama kijiji kinawataka wakazi hao kuwafukuza wanyama hao wakati wanafanya utaratibu wa kulifikisha suala hilo kwenye ngazi husika kwa kuwa sheria haziruhusu kuwaua wanyama hao
Wilaya ya Makete ni miongoni mwa wilaya yenye hifadhi ya taifa amapo inaamnika wanyama hao waharibifu wa mazao hutokea humo na kwa mujibu wa sheria hairuhusiwi kuwaua wanyama hao

No comments:

Post a Comment