Monday, November 19, 2012

ASASI ZILIZOPO WILAYANI MAKETE ZASHAURIWA KUWASHIRIKISHA WATAALAMU WAKATI WA KUPANGA MIRADI




Asasi zisizo za kiserikali wilayani Makete zimeshauriwa kuwashirikisha wataalamu wakati wa uanzishwaji wa miradi mbalimbali ili kupewa ushauri wa kitaalam utakaoweshesha miradi hiyo kufanikiwa kama walivyopanga
Rai hiyo imetolewa kwenye kikao cha wadau wa shirika la MASUPHA kilichofanyika kwenye ukumbi wa shirika hilo kwa lengo la kuona ni namna gani shughuli zinazofanywa na shirika hilo zitafanikiwa zaidi
Akichangia hoja kwenye kikao hicho afisa maendeleo ya jamii wilaya ya Makete Bw. Focus Mwita amesema kuwa mashirika mengi yaliyoanzishwa wilayani hapo mengi yamekufa kutokana na kuanzisha miradi ambayo whawakuwashirikisha wataalamu hiyo malengo hayakutimia hali iliyosababisha ukomo wa mashirika hayo
“Unakuta shirika linaanzisha tuseme mradi wa kuku kwa wanachama wake, sasa badala ya kumchukua Afisa mifugo na akashirikishwa kwanza kuona kama kuku hao watafaa kwa muda huo ama vipi, na kama kuku hao watanunuliwa mbali je wataweza kuishi Makete? Hili litasaidia sana kufanikisha kwa miradi hiyo” alisema Mwita
Pia Mwita ameshauri asasi hizo kufanya upembuzi yakinifu kuwa ni sehemu gani mashirika mengine hayajajikita kusaidia jamii ile ili sehemu kama hizo zipelekewe miradi hiyo ili kuepuka suala la asasi nyingi kufanya shughuli kwenye maeneo yale yale huku mengine yakikosa miradi
Kwa upande wake mratibu wa Ukimwi wilaya ya Makete Dkt. Shadrack Sanga amesema kuwa kwa kuwa shirika hilo la MASUPHA limeamua kuibua mradi wa kutoa elimu ya VVU kwa walemavu, kwa wakati mwingine lione ni namna gani ya kusaidia mahitaji mengine ya walemavu ikiwemo fimbo kwa ajili ya walemavu wasioona ama baiskeli kwa walemavu wa miguu
Amesema wakati mwingine wanapofanya tathmini kwa walemavu huko vijijini wapo baadhi ya walemavu ambao kwa namna nyingine ulemavu wao unaweza kupona endapo watapatiwa matibabu na wataalam, hivyo ni vyema shirika hilo likaona ni namna gani ya kuwaunganisha na hospitali ya CCBRT kwa matibabu zaidi
Katika hatua nyingine msemaji baadhi ya wanavikundi wa MASUPHA ambao walinufaika na mradi wa mbuzi uliotolewa kwao hivi karibuni na shirika hilo wameshauri kupatiwa elimu zaidi ya namana ya kuwatunza`mbuzi hao wa kisasa kutoka kwa wataalamu wa mifugo ili lengo la kupatiwa mradi huo lifikiwe kikamilifu
Mkurugenzi wa shirika hilo Bi. Aida Chengula amesema ao kama shirika wamechukua mapendekezo waliyopatiwa na wadau hao na kuahidi kuyafanyia kazi kwa kushirikiana na wafadhili wao huku akiwataka wananchi wanaoletewa miradi hiyo kuhakikisha inafanikiwa licha ya changamoto za hapa na pale
Amesema ni vigumu kutimiza mahitaji ya watu kwa mara moja lakini kwa kupitia miradi inayoendeshwa na shirika hilo itasaidia kutatua kero za wananchi hao kwa kiasi kikubwa

No comments:

Post a Comment