Ukarabati wa barabara za mitaa katika kijiji cha Utanziwa
kata ya Bulongwa wilayani Makete umefanywa na wakazi wa kijiji hicho ili kujiletea maendeleo kijijini hapo baada ya kutegemea selikari pekee
Akizungumza na mwandishi wetu ofisini kwake Afisa mtendaji
wa kijiji hicho Bwana Paulo Chaula amesema zoezi hilo linafanya na nguvu za wananchi wa kijiji
hicho hadi kumalizika kwake
Amesema ukarabati huo ambao ni upanuzi wa barabara hizo
umeanzia Zahanati ya Utanziwa hadi shuleni
Amesema ingawa wananchi hao hawakuwa na vifaa vyote
vinavyohitajika wakati wa kufanya kazi hiyo lakini anashukuru kuwa zoezi hilo limefanikiwa huku
akiitaka serikali kutembelea kijijini hapo kukagua shughuli za maendeleo
zinazofanywa na wananchi wake
Na Hadija Sanga
No comments:
Post a Comment