Monday, November 12, 2012

TAIFA STARS KUIVAA HARAMBEE STARS KESHO KUTWA

Kikosi cha Taifa Stars kilichoifunga Gambia 2-1 

 
KIKOSI cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kimeingia kambini leo mjini Mwanza kujiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Kenya, Harambee Stars Jumatano, Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Wachezaji walioitwa kwenye timu hiyo ni makipa Juma Kaseja (Simba SC) na Deogratius Mushi ‘Dida’ wa Azam FC.
Mabeki; Kevin Yondan (Yanga), Aggrey Morris, Erasto Nyoni (Azam FC), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Nassoro Masoud ‘Cholo’, Shomari Kapombe na Amir Maftah (Simba).
Viungo; Salum Abubakar ‘Sure Boy’ (Azam FC), Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto, Ramadhan Singano ‘Messi’ na Mrisho Ngassa (Simba), Athuman Iddi ‘Chuji’, Frank Domayo (Yanga) na Shaaban Nditi (Mtibwa Sugar).
Washambuliaji; John Bocco ‘Adebayor’ (Azam FC), Simon Msuva (Yanga), Christopher Edward (Simba), Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wa (TPM, DRC).
Wachezaji wote hao tayari wapo kambini katika hoteli ya La Kairo, maeneo ya Kirumba na leo wamefanya mazoezi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini humo tayari kwa mchezo huo ulio kwenye kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

No comments:

Post a Comment