Dodoma
SERIKALI jana ilishindwa kujibu swali bungeni juu ya mlo kamili kwa wafungwa na mahabusu lililoulizwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema).
SERIKALI jana ilishindwa kujibu swali bungeni juu ya mlo kamili kwa wafungwa na mahabusu lililoulizwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema).
Hata hivyo, kulitokea mgongano katika jibu la
swali hilo kwani Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya ndani, Pereila
Silima awali alishasema wanakula mara tatu jambo lililoonyesha kupingwa
na Waziri wake Dk, Emanuel Nchimbi.
Katika swali lake la nyongeza lililoelekezwa kwa
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Zitto alitaka kauli ya Serikali kama
wafungwa na mahabusu wanapata chakula mara ngapi kwa siku.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk Nchimbi,
alijibu kwa mkato swali hilo na kusema “Taratibu za kazi hazitamkwi
bungeni hivyo kuna mamlaka kamili na maeneo ambayo yanaweza
kuzungumziwa.”
Katika swali la msingi, Jaku Hashim Ayub (Baraza
la Wawakilishi-CCM) alitaka kujua Serikali inatenga kiasi gani kwa mwaka
kwa ajili ya huduma za chakula kwa mahabusu na vituo vya polisi
Zanzibar.
Mbunge huyo alihoji pia iwapo Serikali itakuwa na
taarifa kuwa askari kulazimika kukopa au kutumia fedha zao kuwanunulia
mahabusu chakula na huduma nyingine licha ya kuwa mishahara yao ni
midogo.
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi, Pereila Ame Silima alisema kuwa kiasi cha fedha kinachotengwa
kwa ajili ya kulisha mahabusu kwa nchi nzima hutofautiana mwaka hadi
mwaka kutegemea na ukomo wa bajeti ya wizara.
“Kwa mfano, mwaka wa fedha 2009/10 vituo vya
polisi Zanzibar vilitengewa Sh130 milioni na mwaka 2010/11 Sh100 milioni
zilitengwa kwa ajili ya kazi hiyo.
Kuhusu taarifa za askari kununua chakula kwa ajili
ya wafungwa na mahabusu kwa kutumia fedha zao, alisema Serikali haina
taarifa hizo hadi sasa kwani jukumu hilo ni la Serikali wakati wote.
No comments:
Post a Comment