Natishaaa...! Peter
Odemwingie akishangilia goli alilofunga dhidi ya Southampton
wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England mjini West Bromwich, jana
Novemba 5,
2012.
|
Peter
Odemwingie wa West Bromwich Albion (kulia) akifunga goli dhidi ya
Southampton
wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England mjini West Bromwich, jana
Novemba 5,
2012.
|
LONDON, England
PETER Odemwingie alifunga mara
mbili kuisaidia West Bromwich Albion kuendeleza mwanzo wao mzuri msimu
huu kwa
ushindi wa 2-0 dhidi ya timu inayoburuta mkia ya Southampton na kukwea
hadi
katika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England jana.
Shuti la mshambuliaji Odemwingie
katika dakika ya 36 lilifungua akaunti ya magoli ya wenyeji na Mnigeria
huyo
akaongeza jingine katika dakika ya 60 baada ya kuunganisha vyema kwa
kichwa cha
karibu na lango krosi ‘kali’ ya Shane Long.
West Brom wana pointi 17 kutokana
na mechi 10, sawa na timu inayokamata nafasi ya nne ya Everton na saba
nyuma ya
vinara Manchester United.
Southampton wamejikusanyia pointi
nne, sawa na Queens Park Rangers ambayo haijawahi kushinda, lakini wako
mkiani
mwa msimamo wa ligi kutokana na tofauti ya mabao.
West Brom wamepoteza pointi
katiika mechi zao mbili zilizopita dhidi ya mabingwa Manchester City na
pia Newcastle
United, kwa kuruhusu magoli ya dakika za majeruhi lakini safari hii
hawakufanya
makosa dhidi ya kikosi cha Southampton.
Zoltan Gera alipoteza nafasi ya
wazi katika dakika ya 20 wakati shuti la Odemwingie lilipokwenda moja
kwa moja
miguuni mwake lakini akiwa umbali wa yadi sita kutoka golini akapiga
shuti
lililopaa juu ya lango.
Baada ya goli la utangulizi la
Odemwingie
lililotokana na shuti lililomparaza Maya Yoshida na kumpita kipa Paulo
Gazzaniga, Southampton walikosa bahati ya kusawazisha baada ya shuti la
Rickie
Lambert kugonga ‘besela’ mwanzoni mwa kipindi cha pili.
Kipa wa West Brom, Ben Foster
alifanya
kazi nzuri ya kuokoa na kuinyima Southampton goli katika muda wa
majeruhi.
Odemwingie alifurahishwa na
kiwango cha timu yake baada ya kupata vipigo katika dakika za majeruhi
kutoka
kwa Man City na Newcastle.
"Haya yalikuwa majibu mazuri
kutoka kwa timu nzuri. Tulihitaji bahati kidogo na ni rahisi, kama
mkiendelea
kupiga mashuti mtafunga, tumefurahi kupata pointi zote tatu," Odemwingie
aliiambia
Sky Sports.
No comments:
Post a Comment