Rai imetolewa kwa mashirika na watu binafsi kuwasaidia
watoto yatima wanaosoma katika shule ya msingi Ivalalila wilayani Makete, kama namna mojawapo ya kuwafariji kutokana na watoto hao
kupoteza wazazi wao
Rai hiyo imetolewa na mwalimu mkuu wa shule hiyo Bw. Nathan
Komba wakati akizungumza na mwanahabari wetu ofisini kwake
Mwl. Komba amesema kati ya wanafunzi 398 wanaosoma shuleni
hapo, miongoni mwao 90 ni yatima hivyo wanahitaji faraja kutoka kwa jamii
Akizungumzia watoto hao yatima mwalimu huyo amesema wengi
wao mahudhurio shuleni si ya kuridhisha kutokana na sehemu wanazoishi na wakati
mwingine siku ya alhamisi ambayo ni ya gulio wengi wao hushindwa kufika shuleni
na badala yake huenda kuuza mkaa gulioni ili wajipatie kipato
Amesema hali hiyo hupelekea watoto hao kutofanya vizuri
katika mitihani yao
kwani wanapitiwa masomo kutokana na kutofika shuleni kuhudhuria masomo, hivyo
kuiomba jamii na mashirika mablimbali kuwasaidia waoto hao hasa kwa kuwapatia
mahitaji ya shule
Na Hadija Sanga
No comments:
Post a Comment