Wahanga wa mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali katika halmashauri
ya Njombe Mji, wameanza kukarabati nyumba zao bila kupata msaada
wowote kutoka serikalini.
Mwandishi wa mtandao huu alishuhudia wakazi wa mitaa mbalimbali ambayo
nyumba zao zilizoathirika na upepo huo kwa kuezuliwa paa na nyingine
kuanguka, wakikarabati nyumba zao tayari kwa kuendelea na maisha yao.
Wakizungumza na www.gabrielkilamlya.blogspot.com wananchi hao kwa nyakati tofauti walisema
mpaka sasa hawajapata msaada wowote kutoka serikali, na kuiomba
serikali ya wilaya ya Njombe kuwasaidia kwa kuwapatia msaada chakula
na mahitaji mengine mhimu.
“Mwanangu kama unavyoniona mimi na uzee wangu niko hapa peke yangu
sina mtu wa kunisaidia, nimeamua kuuza ndama wangu nikapata fedha
kidogo ndiyo iliyonisaidia kununua mabati mapya matano, haya hapa
unayoyaona, lakini kwa kuwa sina uwezo nimeamua kuchanganya mapya na
haya makuukuu yaliyochoka kama unavyoyaona,” alisema Lunanilo
Kihindo(76) mkazi wa mtaa wa Kibena.
Aliitaka serikali na wadau mbalimbali kuwasaidia kwa kuwa mafurikio
hayo yamewaathiri kwa kiasi kikubwa na kurudisha nyuma maendeleo yao,
kwani vitu mbalimbali ikiwemo chakula viliharibiwa na mvua hiyo.
Naye Lucia Nyongole mkazi wa kijiji cha Nundu aliitaka serikali
kufanya mchakato wa kuwasaidia haraka kwa kuwa shida wanayoipata kwa
sasa ni kubwa.
“Kwa kweli ninaiomba serikali itusaidie sisi wananchi wake haraka, kwa
kuwa kwa sasa hatuna makazi na tunalazimika kuishi kwa majirani,”
alisema Lucia.
Kwa upande wake Lufina Mlowe mkazi wa Nundu ambaye ni shuhuda wa
maafa hayo, aliitaka serikali kuwa na mfuko wa dharura wa maafa katika
halmashauri badala ya kutegemea ofisi ya waziri mkuu kitengo cha
maafa, ili pale yanapotokea maafa ya aina yoyote wananchi waweze
kusaidiwa haraka.
“Tungekuwa na mfuko wa dharura katika halmashauri ungewasaidia
wananchi waliopatwa na maafa haya wakati wakisubiri huo msaada
mwingine kutoka serikali kuu,” alisema Mlowe.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Njombe Mji George Mkindo,
alikiri waathirika hao mpaka sasa kutopata msaada wowote kutoka
serikalini, kwa kuwa serikali ilikuwa bado haijakamilisha zoezi la
kufanya tathmini juu ya maafa hayo.
Hata hivyo alisema zoezi hilo kwa sasa tayari limekwishakamilika, na
kubaini kuwa uharibifu uliosababishwa na mvua hiyo umesababisha hasara
ya zaidi sh. 41 milioni, ambayo inatokana na uharibufu wa nyumba 178,
vyakula pamoja na mazao mbalimbali shambani.
“Hasara iliyopatikana kutokana na uharibifu wa mvua hiyo ni zaidi ya
sh. 41 milioni, ambayo imetokana na uharibifu wa nyumba 178, vyakula
pamoja na mazao shambani,” alisema Mkindo.
Alisema kwa kuwa sasa tathmini hiyo imekwishakamilika na thamani
halisi ya uharibifu huo kubainika, ataituma taarifa hiyo katika ofisi
ya Waziri Mkuu kitengo cha maafa haraka iwezekanavyo, ili wahanga wa
maafa hayo waweze kupatiwa msaada.
Hata hivyo alitoa wito kwa wananchi wa mitaa na vijiji vivyokumbwa na
maafa hayo kuendelea kusaidiana na wahanga wa maafa hayo katika
shughuli za ukarabati wa nyumba na mahitaji mengine mhimu, wakati
wakisubiri msaada kutoka serikalini.
Mafuriko hayo yalitokea usiku wa kuamkia Novemba 09 mwaka huu na
kuziacha kaya zaidi ya 170 bila makazi baada ya nyumba zao kuanguka na
kuezuliwa paa, huku nyingine zikionekana zikiwa zimeangukiwa na miti.
Mitaa iliyoathiriwa zaidi na mvua hizo, ni Kibena, Ramadhani, Kihesa
na Kijiji cha Nundu kilichopo nje kidogo ya Mji wa Njombe.

No comments:
Post a Comment