Saturday, October 27, 2012

CCM YAFANYA MASHAMBULIZI MAKETE




Chama cha mapinduzi wilaya ya Makete kimeendelea kujihimalisha kuhakikisha wanateea kiti cha udiwani kata ya Luhumbu wilayani hapo baada ya kufunga akmpen hii leo
   Mtandao huu umeshuhudia baadhi ya vingozo wa chama hicho waakiwemo Naibu waziri Maji Mh binlith Mahenge ambaye pia ni mbuge wa wilaya wengine ni Mwenyekiti  Katibu wa chama hicho pomoja na baadhi ya madiwani walikuwepo kwenye msafara huo
  Uongozi wa chama hicho umefanya mkutano wa kufunga kampen hizi katika kijiji cha Usililo katika kata hiyo akihutubia wakazi wa maeneo hayo Mh mahenge amesema wananchi wasidanganyike na vyama vingine badala yake wamchague Enok Ngailo kupitia ccm nakuongeza kuwa tayari chama hicho kimesha waletea barabara pamoja na maji katika kijiji hicho  pamoja na miradi mingine iliyopo katika hatua ya utekelezaji .
  Naye katibu wa chama hicho bwana Milaji mtaturu (jembe)amesema kuwa chama hicho kimeshaanza utekelezaji wa ilani  ya chama hicho za mwaka 2010hadi 2015 hivyo ni vema wakaipa ccm ili iweze kumalizia utekelezaji wa irani hiyo na kueleza jinsi wa Tanzania wengi wanavyo angamia kwakukosa maarifa
   Uchaguzi huu nafanyika baada ya kifo cha aliyekuwa wa kata hiyo bwana Sanga na uchaguzu huo utafanyika kesho jumapili
  Katika hatua nyingine msimamizi wa uchaguzi huo Bwana Kapinga amesema kuwa uchaguzi unatarajia kufanyika kesho huko luhumbu  na tayari vifaa vya uchaguzi wamepokea na tayari suala la ulinzi na usalama hapo kesho upo sawia na amewataka wananchi kutofanya vitendo vyovyote vya uvunjifu wa amani badala yake wafuate kanuni na sheria za uchaguzi
    


No comments:

Post a Comment