Tuesday, December 3, 2013

ULEVI TATIZO LA UKIMWI MAKETE




Wananchi wilayani Makete wameaswa kuachana na Ulevi wakupindukia ili kujiepusha na maambukizi ya virusi vya ukimwi hatimaye kuishusha Makete katika maambukizi ya ukimwi na hatimaye kuisha kabisa
Hayo yamesemwa na mkuu wawilaya ya makete mh josophine Matiro katika maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani yaliyo fanyika kiwilaya katika kata ya mbalatse
Aidha mkuu wa wilaya hiyo amekemea vitendo vya wanaume kuridhi wajane kwani imeonekana kuwa wananchi wengi huwa wanawarithi wajane bila kujua afya zao 

''Wanaume wengi mnawarithi wajane ikiwa hamjui ni magonjwa gani ambayo mjane huyo anaishi nayo na baadaye unaambiwa ukapime hutaki,kutumia dawa hutaki na badala yake unaanza kudai serikali haitusaidii katika huduma ya wanaoishi kwa matumaini wakati hutaki kutumia dawa wewe mwenyewe,tambua kuwa Ugonjwa wa ukimwi ni ugonjwa hatari sana''

Aidha katika hatua nyingine wananchi hao kupitia kwa Mh.Diwani wao Bw.Msingwa wameuomba uongozi wa Halmashauri ya wilaya kuwasaidia katika kikundi cha mama na mtoto kuwapatia ng`ombe wa maziwa ili waweze kujikwamua na umasikini ambapo Mkurenzi wa Wilaya ameahidi kukisaidia kikundi hicho

No comments:

Post a Comment