Umati wa wananchi waliokusanyika kumsikiliza Dk. Slaa siku ya jana mjini Kasulu Uwanja wa Kiganamo kabla ya mkutano kuvunjika.
Mkutano wa Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), Dk Willbroad Slaa uliofanyika Uwanja wa Kiganamo, Kasulu
Mjini siku ya jana umevunjika baada ya polisi kupiga mabomu ya machozi
wakikabiliana na vijana waliorusha mawe kupinga mkutano usiendelee. Kwa
mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, vijana hao wanadaiwa kuwa kati ya 10-15
ambao walirusha mawe baada ya wananchi kuwafukuza wakitaka kuwapiga
wakipinga kitendo chao cha kupiga kelele ili mkutano usiendelee ndipo
polisi walianza kulipua mabomu ya machozi na mkutano kuvunjika.
No comments:
Post a Comment