Sunday, December 8, 2013

HUYU NDIO MSHINDI WA TUSKER PROJECT FAME 6 MWAKA 2013

 

Mshiriki Hope toka Burundi amejikuta akianguka chini kwa mshituko wa furaha ulimkuta baada ya kuibuka kidedea kwa kutangazwa mshindi wa Tusker Project Fame na kujinyakulia kitita cha Shilingi 5,000,000/= za Kenya .

Mashindano hayo yaliyomalizika hivi punde usiku huu yamemwacha Hope katika taharuki huku akiwabwaga wenziye; Hisia (Tanzania), Patrick (Rwanda),Wambura (Kenya), Daisy (Uganda),Amos & Josh wa Kenya(Pichani chini).

Sauti ya pekee ya kijana huyo imeibua thamani yake katika tasnia ya muziki,Hope hakuwahi kufanya video shooting ya wimbo wowote zaidi ya ule uliompatia ushindi wa Tusker.
Tembelea You-tube kuona yaliyojiri katika mashindano hayo.

No comments:

Post a Comment