Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Masoko ,kijiji
cha Lupando wilaya ya Rungwe ,Katibu Mkuu waliwaambia wananchi hao kuwa
urasimu na umangi meza wa watendaji wa serikali ndio unachangia kwa
kiasi kikubwa kurudisha maendeleo yao nyuma na kusema kamwe CCM
haitokubali hali hiyo iendelee na kusisitiza CCM itahakikisha wananchi
wanapata haki zao za msingi kwanza.
Mwakilishi wa
Wananchi wa Kijiji cha Lupando Ndugu Wema Mwaipopo akiomba sana kwa
niaba ya wananchi wake watatuliwe suala la maji,umeme na barabara kwani
hizo ndio zilikuwa ahadi kubwa za Mbunge na Rais.
Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Masoko kijiji
cha Lupando na kuwaambia wananchi kuwa wapinzani ni sawa na Jogoo hata
aamke saa ngapi hawezi fungua mlango,na kuwasisitiza wananchi wa kijiji
hicho ni CCM pekee inayoweza kuwazungumzia na kero zao zikatatuliwa.
Asumwisi
Asagwile Mwatebela ,Mlezi wa Vijana wa Chadema wilaya ya Rungwe
akirudisha kadi yake kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na
kujiunga rasmi na CCM.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Kiwira Rungwe na
wakati wa ufunguzi wa vikundi viwili vya wajasiriamali ambapo aliwaambia
vijana maendeleo yanaletwa kwa kufanya kazi kwa kujituma na waondoe
mawazo kuwa Katiba mpya ndio itakuwa mwarobaini wa matatizo yao.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia maabara ya shule ya Sekondari ya
Ikuti ikiwa moja ya sehemu ya ahadi ya serikali ya kujenga maabara
katika kila shule ya Sekondari ya Kata.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa Nyumba za walimu wa shule ya Sekondari Ikuti wilayani Rungwe.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahmani Kinana akiongozana na Mkuu wa Shule ya Ikuti
Ndugu Emmanuel Ngasa pamoja na viongozi wengine wa chama na serikali
baada ya kukagua jengo la hosteli la shule ya sekondari ya Ikuti.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wakazi wa shina namba
2,Butonga Tawi la Ikuti kwa Balozi James Mbasi, na kusisitiza viongozi
wote wa CCM waige mfano wa Mabalozi kwani wanafanya kazi kwa kujitolea
katika kukiimarisha na kukijenga chama.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahama Kinana akikata utepe kama ishara ya kuwasha umeme
katika kituo cha Afya cha Ikuti wilayani Rungwe.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na viongozi wa wilaya ya Rungwe
pamoja na wananchi kuelekea kwenye uwanja wa mkutano Ikuti.
Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya Wilaya Ndugu Richard Kasesela akipiga ngoma ya
Kitongo kabla ya kuanza kwa mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Ikuti
ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Mbunge wa Viti
Maalum Wananwake mkoa wa Mbeya Dk.maru Mwanjelwa akicheza ngoma kabala
ya kuanza kwa mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Ikuti ambapo Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na viongozi wa kitaifa
aliofutana nao Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose
Migiro na Katiibu wa NEC Itikadi na Uenezi walihutubia.
Mbunge wa Viti
Maalum Mkoa wa Mbeya Dk.Mary Mwanjelwa akihutubia wakazi wa kata ya
Ikuti na kuwaambia wanawake waandae vikundi vyao kwani Benki ya wanawake
karibia itafunguliwa hivyo fursa za kupata mikopo zitaongezeka na
kusaidia kufanya biashara kwa ufanisi na kuleta maendeleo.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Ikuti wilayani Rungwe
mkoa wa Mbeya na kusema serikali ipunguze matumizi yasiyo na lazima na
badala yake nguvu nyingi iletwe kwa wananchi katika kuwaletea maendeleo.
Wakazi wa Ikuti
wakiwa juu ya mti wakisikiliza kwa makini hotuba za viongozi wao ambazo
nyingi zilijibiwa vizuri hasa suala la umeme ambalo wananchi wanaweza
kulipa kidogo kidogo.
Dk.Mary mwanjelwa
akizungumza na akina Mama wauza ndizi wa kijiji cha Iponjola kata ya
Rufingo wilaya ya Rungwe na kuwataka waanzishe vikundi kwani benki ya
wanawake ipo karibuni kufunguliwa katika mkoa wa Mbeya hivyo itawasaidia
kupata mikopo kwa riba nafuu.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alisimama kuwasalimu wakina mama hao kisha
kuutambulisha uongozi wote aliokuwa nao kwenye msafara.
No comments:
Post a Comment