Tukio la mauaji ya mvuvi, lilitokea juzi
katika Kijiji cha Itindi wilayani Chunya.
Mvuvi aliyeuawa alitajwa kwa jina la Hatibu Mwakalinga(36),
ambaye aliuawa kwa kupigwa na fimbo mbavuni na wachunga Ng’ombe wafugaji wa
kabila la kisukuma.
Imeelezwa kuwa marehemu alikuwa na kundi la
Sungusungu wakikamata mifugo mali ya wafugaji waliofahamika kwa jina mojamoja
la Mwanahela, Kabahungu na Lukangila.
Tukio la pili lilitokea jana katika Kijiji
cha Mshewe kata ya Utengule Usongwe wilaya ya Mbeya Vijijini, ambapo watoto
wawili walikufa kwa ajali ya moto baada ya nyumba yao kuungua.
Waliofariki dunia ni Desmos Raphael(2) na
Dorcas Raphael mwenye umri wa miezi minne.
Chanzo cha tukio
hilo ni baada ya mama mzazi
wa watoto hao Floiza Emmanuel(20), ambaye alikuwa amelala na watoto
wake, kisha kutoka nje majira ya saa sita usiku kujisaidia na kuacha
amewasha kibatari, na
aliporudi akakuta nyumba yake inawaka moto.
Kamanda wa polisi mkoani Mbeya, Diwani
Athumani amethibitisha kutokea kwa matukio yote mawili na ametoa wito kwa
wachunga mifugo waliosababisha kifo cha mvuvi wilayani Chunya kujisalimisha.
No comments:
Post a Comment