BENKI ya NMB
tawi la Tukuyu wilayani Rungwe mkoani Mbeya, imelalamikiwa kuwashawishi kutoa
rushwa wajasiliamali wanaohitaji mikopo katika tawi hilo.
Wakizungumza namwandishi wa blog hii wajasiliamali hao
walisema kuwa wamekuwa wakikopa na kurejesha vema mikopo yao lakini tangu May
mwaka huu, wamezuiliwa na uongozi wa benki hiyo.
Mjasiliamali
Habakuki Mbwilo, alisema yeye mwaka jana alikopa 3 Milioni na kurejesha kwa
riba ya Shilingi laki tatu na elfu Hamsini, lakini kwa sasa amezuiliwa pamoja
na wenzake kwa madai kuwa akaunti yake haina mzunguko mzuri wa fedha.
‘’Mfano ukitaka
kukopa Milioni tatu, unaambiwa kuwa unatakiwa uwaachie Shilingi Laki tano
lakini deni lako linakuwa pale pale jambo ambalo tunashindwa, hatuna kwa
kukimbilia na tunaiomba serikali iingilie kati jambo hili’’ alisema Mbwilo.
Alisema hali
hiyo imekuwa kero hata kwa baadhi ya watumishi wa kitengo cha mikopo cha benki
hiyo ambao alisema kuwa nao wanasema hawana namna ya kuwasaidia wajasiliamali
hao kutokana na maagizo ya meneja wao ambaye amebakiza miaka michache kustaafu.
‘’Hatujawahi
kuchelewesha kurejesha wala kukiuka masharti ya mkataba wa mkopo lakini
wameamua kutufungia, hatujajua kama labda sera ya serikali imebadilika’’
walisema wajasiliamali hao.
Tanzania
daima liliwasiliana kwa njia ya simu na Mkuu wa wilaya ya Rungwe Crispin Meela
ambaye alisema kuwa hakuwa na taarifa hiyo.
‘’Sijapata malalamiko
hayo lakini nawaomba kama wanayo
malalamiko hayo waje nitashughulikia haraka iwezekanavyo….’’ Alisema Meela.
Wajasiliamali
hao wanaolalamikia benki hiyo ni pamoja na wanaofanya biashara za urembo, viatu
na vipodozi katika mji wa Tukuyu.
No comments:
Post a Comment