Wednesday, July 31, 2013

WAFUGAJI WATAKA KATIBA MPYA KUWARUHUSU KUUA SIMBA WANAOVAMIA MIFUGO YAO


Wafugaji  wakazi wa Mlowa  jimbo la Isimani  mkoa  wa Iringa  wakiwa katika mkutano wa kukusanya maoni ya katiba  mpya jana
Mfugaji  akitoa maoni yake  juu ya katiba  mpya  na  kulalamikia  simba  wanaoua mifugo  yao
Mwenzeshaji  Happy Kikoga  kutoka  kituo cha msaada cha sheria na  haki  za  binadamu akiwasomea  rasimu  ya  katiba wananchi  wa Mlowa Isimani
Mmoja kati ya  wanawake  wakazi wa Mlowa  akichangia katika mkutano huo kwa  kutaka  wanaopandikiza chuki  za kidini  kupewa adhabu kali.

WAFUGAJI jamii ya  kimasai na Mang'ati  wakazi  wa Mlowa  jimbo la Isimani  wilaya ya  Iringa  vijijini mkoani Iringa  wametaka katiba mpya ijayo  kuwaweza kuwatetea wafugaji kwa  kuingiza  kipengere  kitakachowaruhusu  wao  kuingia katika  hifadhi ya  Taifa ya  Ruaha  kuwasaka  simba  wanaoua mifugo  yao  kuwaua  .


Wafugaji  hao  walitoa  maoni hayo juzi  katika  ofisi  za serikali ya  kata  wakati  wakichangia rasmu ya katiba mpya  zoezi lililoendeshwa na kituo  cha  msaada cha sheria na  haki  za  binadamu.


Walisema  kuwa  Simba  wameendelea kuwatesa na  kila  wakati  wanaendelea  kuua mifugo yao na  pindi  wanapofanya msako  wa  kuwasaka  askari  wa  wanyamapori  wanawachukulia hatua  kali .


Hivyo  walisema  ili  katiba  ijayo  iweze kutambua haki za  wanyama  wengine na  pia  kutambua  uwepo  wa  wafugaji ni  vema kuingizwa  kipengere  kinachowapa nafasi  ya  kuwaua  simba wanaokula  wanyama  wao.


Mbali ya  kutaka  kuwekwa kwa  kipengere  hicho  bado  wafugaji hao  walitaka  kutambuliwa  rasmi  na katiba  ijayo badala  ya ilivyo sasa  ambapo  wamekuwa wakihamishwa  kama  wanyama .

Pamoja na  wafugaji hao kwa upande  wake wananchi  wa kawaida  wameeleza  kusikitishwa na hatua  iliyofikiwa ya mchakato  huo wa katiba  mpya  hatua ya  kukusanya maoni  juu ya rasmu wakati  wao hata katiba  iliyopita  hawaijui na rasmu  hiyo  hawajapata  kuoina .

No comments:

Post a Comment