Tuesday, July 30, 2013

UHALIBIFU WA VYANZO VYA MAJI WAENDELEA MBOZI


VYANZO VYA MAJI VILIVYOPO KATIKA KATA YA VWAWA WILAYANI MBOZI MKOANI MBEYA VINAKABILIWA NA UHARIBIFU MKUBWA WA MAZINGIRA UNAOFANYWA NA WAKAZI WA VIJIJI VYA ILEMBO NA HASAMBE KATIKA KATA HIYO.

UHARIBUFU UNAOFANYIKA  KATIKA VYANZO HIVYO NI UKATAJI WA MITI KWA AJILI YA UCHOMAJI WA MKAA, KUKATA KUNI NA KUENDESHA KILIMO CHA BUSTANI KATIKA KINGO ZA MTO VWAWA NA MANTENGA AMBAYO NDIO VYANZO PEKE VYA MAJI KATIKA ENEO HILO.

DIWANI WA KATA YA VWAWA RICHARD KIBONA AMEIAMABIA RADIO FREE AFRICA MINI MBOZI KUWA UHARIBIFU HUO UMEPELEKEA KUPOTEA KWA MAZINGIRA ASILIA YA ENEO HILO HUKU KUKIWA NA HATARI YA ENEO HILO KUWA KAME KATIKA SIKU ZIJAZO.

AMESEMA AMEKUWA AKIFANYA  JITIHADA  ZA KUWASILIA NA WATAALAMU WA MALI ASILI NA MAZINGIRA PAMOA NA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA HIYO JUU YA UHARIBIFU HUO LAKINI HAKUNA HATUA ZILIZO WAHI KUCHUKULIWA ZAIDI YA WAKUU WA IDARA HUSIKA KUFIKA ENEO LA TUKIO  KWA AILI YA UKAGUZI NA KUONDOKA.

KIBONA AMEIOMBA HALMASHAURI YA WILAYA HIYO KWA KUSHIRIKIANA NA VIONGOZI WA KATA NA VIIJI KUFANYA MKUTANO WA HADHARA NA WANANACHI WA KATA HIYO ILI KUWAELIMISHA ATHARI ZA UHARIBIFU HUO SANJARI NA UMUHIMU WA UTUNZAJI WA MAZINGIRA VIKIWEMO VYANZO HIVYO VYA MAJI.

No comments:

Post a Comment