Tuesday, June 4, 2013

MWANDISHI WA HABARI ABSALOM KIBANDA KUREJEA TANZANIA LEO








MWENYEKITI wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda anatarajia kuwasili leo akitokea nchini Afrika Kusini alipokuwa akitibiwa tangu Machi 6, baada ya kushambuliwa na kuumizwa vibaya na watu wasiofahamika usiku wa Machi 5.

Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu wa TEF, Neville Meena, Kibanda atawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere leo saa 7 mchana na atazungumza na waandishi wa habari.
Kutokana na ujio huo, Meena aliwaomba wahariri na waandishi kufika uwanjani hapo kuanzia majira ya saa 6.00 mchana kwa ajili ya kumpokea mwenzao huyo aliyekaa nje ya nchi kwa miezi mitatu.
“Mwenzetu kakaa Afrika Kusini kwa siku 90, hii ni fursa nyingine adhimu ya waandishi wa habari nchini kuonyesha mshikamano na umoja wetu kwa kwenda kumpokea,” alisema.
Kibanda ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa New Habari (2006) Ltd, kuumizwa kwake kuliitikisa tasnia ya habari nchini na kuzua mijadala mbalimbali ndani na nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment