Tuesday, June 4, 2013

ANUSURIKA KUUWAWA KWA KUBAKA MTOTO WA MIAKA 10




WAKATI mkoa wa Iringa ukiwa ni mkoa wa pili kwa maambukizi ya virusi vya UKIMWI ukiwa nyuma ya mkoa wa Njombe ambao ndio unaongoza huku vitendo vya ubakaji na mapenzi yasiyo salama vikitajwa ni sababu ,Jemba mmoja mkazi wa Mwangata katika Manispaa ya Iringa amenusurika kuuwawa na wananchi wenye hasira kali baada ya kubambwa akibaka kitoto cha miaka 10 mchana kweupe.

Mashuhuda wa tukio hilo wameueleza mtandao huu wa www.matukiodaima.com na www.francisgodwin.blogspot.com kuwa tukio hilo limetokea mida ya saa8 mchana baada ya mama mazazi wa binti huyo kusikia mtoto wake akilia kwa uchungu kuomba msaada zaidi kwa wananchi baada ya kukamatwa kwa nguvu na kijana huyo mbakaji




Mama mzazi wa mtoto huyo ambae Jina lake na la mtoto wake kwa sasa yamehifadhiwa na mtandao huu kutokana na sababu za kimaadili ,alisema kuwa wakati tukio hilo likitokea yeye alikuwa akiendelea na shughuli zake nyumbani na kusikia sauti ya mtoto wake akilia kwa uchungu kulalamika kubakwa .

Hata hivyo alisema baada ya kutoka nje na kuelekea eneo hilo ambalo sauti ilisikika alishuhudia kijana huyo akiendelea kumbaka mtoto wake jambo lilopelekea kupiga kelele kuomba msaada kwa wananchi ili kusaidia kumkamata mtuhumiwa huyo wa ubakaji.

Mwanamke huyo alisema kuwa jitihada za wananchi wa eneo hilo la Mwangata kumkamata mtuhumiwa ziliweza kufanikiwa pamoja na mtuhumiwa huyo kutaka kujaribu kukimbia eneo hilo.

Mmoja kati ya wananchi walioshiriki kumkamata kijana huyo mbakaji aliyejitambulisha kwa jina la Samweli kalinga alisema kuwa kijana huyo amekuwa na tabia ya kuwabaka watoto katika eneo hilo la Mwangata na mara nyingi watoto wamekuwa wakibakwa ila walikuwa hawajui ni nani anayeendesha vitendo hivyo vya ubakaji .

Hivyo alisema kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo wa ubakaji kulepelekea wananchi wenye hasira kali kuanza kumwadhibu kwa kichapo na hata kutaka kumchoma moto kabla ya baadhi ya wananchi kutumia busura na kutaka afikishwe kituo cha polisi.


Mtuhumiwa huyo amefikishwa katika kituo kikuu cha polisi mjini Iringa huku akiwa hoi kwa kichapo na kupelekea kuvuja damu kupita kiasi kichwani kutokana na kichapo alichokipata kutoka kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment