Thursday, June 13, 2013

MAFUTA BEI JUU

 Serikali imetangaza bajeti yake ya mwaka 2013/14 na kupandisha ushuru wa mafuta ya petroli na dizeli kwa Sh200.
Katika bajeti ya mwaka 2012/2013, Serikali ilieleza hatua ilizochukua kukabiliana na changamoto zinazowakabili wananchi kwa lengo la kupunguza makali ya maisha kunakotokana na kupanda kwa bei za bidhaa na huduma.
Ilieleza hatua zilizochukuliwa kuwa ni pamoja na kurekebisha namna ya kukokotoa gharama za mafuta na kutangaza bei elekezi kila mwezi na kuanzisha utaratibu wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja.
Akisoma bajeti hiyo jana mjini Dodoma, Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa, alisema mafuta ya dizeli ushuru wake umepanda kutoka Sh215 kwa lita hadi Sh217 ikiwa ni ongezeko la Sh 2 tu.
“Mafuta ya petroli kutoka kiwango cha sasa Sh339 kwa lita hadi Sh400 kwa lita,” alisema.
Alifafanua kwamba mafuta ya taa ushuru wake umebaki kuwa Sh400.30.
Hotuba ya Waziri Dk Mgimwa kuhusu bajeti, itaanza kuchangiwa na wabunge Jumatatu ijayo.
Hata hivyo baadhi ya wananchi, wameelezea hisia zao kuhusu bajeti hiyo wengi wakidai kuwa inawazidishia ugumu wa maisha.

No comments:

Post a Comment