Sunday, June 16, 2013

BOMU LINGINE LAUA ARUSHA





Na Upendo

 
Zaidi ya watu watatu wamekufa na wengine kadhaa kujeruhiwa, katika mlipuko wa bomu uliyotokea katika viwanja vya Soweto mkoani Arusha, wakati wa kuhitimisha kampeni za udiwan za chama cha Demokrasia na maendeleo, Chadema.

Akizungumza na waandishi wa habari, katika hospitali ya seliani kamanda wa Polis Mkoani Humo Bwana Leberatus Sabasi, amesema watu wawili wamekufa katika hospitali ya Celiani na Majeruhi wa tukio hilo wamelazwa katika hospitali hiyo na Maunt Meru mkoani Humo.

Aidha Katika hospitali ya mkoa Mauti Meru, mtu mmoja amekufa, muda mfupi baada ya kufikishwa katika hospitali hiyo.

Viongozi mbalimbali wa chama cha demokrasia na Maendeleo Chadema, akiwemo Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema, Mwenyekiti wa chama hicho Kitaifa Mheshimiwa Freemon Mbowe, wamefika katika hospitali hizo kuangalia hali za majeruhi.

Tukio hilo limetokea majira ya saa kumi na mbili jioni, na kusababisha taharuki na simazi kwa wakazi wa mkoa wa Arusha, waliyokuwa katika mkutano wa chama cha demokrasia na Maendeleo Chadema.

Mwezi ulipita tukio kama hili lilitokea katika kanisa la mtakatifu Josefu Olasiti mkoani Arusha, na kusababisha watu kadhaa kujeruhiwa.

No comments:

Post a Comment