Tuesday, June 11, 2013

HALI YA MANDELA HAIJABADILIKA

 Rais wa zamani wa Afrika kusini, Nelson Mandela, bado yuko hospitalini akipokea matibabu katika chumba cha wagonjwa mahututi baada ya kukumbwa tena na maradhi ya mapafu. Mandela alipelekwa hospitalini siku ya Jumamosi mjini Pretoria. Afisi ya Rais imesema hali yake bado ni mbaya lakini inadhibitiwa. Hii ni mara ya nne kwa kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 94 kulazwa hospitalini tangu mwezi Desemba mwaka jana. Mandela anayeonekana kielelezo cha maridhiano na amani nchini mwake kwa kukomesha ubaguzi wa rangi ana historia ya matatizo ya kupumua tangu apatwe na ugonjwa wa kifua kikuu alipokuwa jela kwa miaka 27.

No comments:

Post a Comment