Na Bazil Makungu Ludewa
WAKATI watanzania,
wazazi, wadau mbalimbali wa elimu na taifa wakitafakari juu ya kutoa motisha na
kutengeneza mazingira mazuri kwa walimu ili waweze kufundisha na kuishi katika
mazingira magumu hasa vijijini, madiwani katika halmashauri ya wilaya ya Ludewa
katika Mkoa wa Njombe wao wamewataka walimu wanaoishio kwenye nyumba za
serikali kuanza kulipia pango mara moja.
Maagizo hayo ya
madiwani katika halmashauri ya wilaya ya Ludewa imekuja muda mfupi huku taifa
likihangaika na kuunda tume ya kubaini na kumtafuta mchawi yupi aliyehusika na
matokeo mabovu ya mtihani wa kidato cha nne mwaka huu.
Kwa mujibu wa barua
zilizosambazakwa walimu wakuu ambazo nakala tunayo, walimu wote wanatakiwa
kulipia nyumba hizo kwa kiwango cha shilingi elfu(10,000) bila kujali ubora
wala uimara wa nyumba hizo na haijalishi kama nyumba hiyo imejengwa kwa kutumia
miti, nyasi, bati au saruji kila anayeishi kwenye nyumba ya serikali pasipo
kujali kama nyumba hiyo iko mjini au kijijini atatakiwa kulipia pango.
Wakizungmza na gazeti
hili kwa nyakati tofauti walimu wa shule za sekondari na msingi wameeleza
kusikitishwa kwao na maamuzi ya madiwani yakuwatoza kodi bila kuangalia uborawa
nyumba zenyewe na kuongeza kuwa kuna nyumba hazifai kuishi binadamu lakini wao
wanavumilia.
Aidha wamesema kuwa
wapo wanaokatwa kodi lakini hawaishi kadhaa, ubabe unaofanywa na madiwani
katika halmshauri ya wilaya ya Ludewa hasa katika masuala mbalimbali bila
kuwahusisha wataalamu waliokaa muda mrefu darasani kupata taaluma zao.
Akijibu
malalamiko ya walimu mwenyekiti wa
halmashauri ya wilaya ya Ludewa Matei Kongo alisema kodi hiyo inawahusu watumishi
wote ndani ya wilaya yake wakiwemo idara ya elimu na afya ili mradi awe anaishi
katika nyumba ya serikali ikiwemo zile nyumba zilizojengwa kwa mpango wa MAM na
MES watalazimika kulipia.
‘’’’’ hakuna mkataba
wowote tuliokubaliana na watumishi kwamba wanapoletwa kuanza kazi lazima
tuwajengee nyumba, mtumishi aliomba kazi na kuingia mkataba na serikali kisha
kuletwa Ludewa kwa ajili ya kufanyakazi kama ajira yake invyosema na si kuishi
bure kwenye nyumba yetu.’’’’’’ Alifafanua Kongo
Tuwe na wazo la
pamoja la kuendeleza nyumba zetu kwa hiyo kila mwalimu anayeishi kwenye nyumba
ya serikali achangie gharama ya hiyo
nyumba ili ikiwezekana tukikusanya kwa mwaka tuweze kujenga nyumba zingine
mahali pengine kwa sababu halmashauri inatakiwa kujitegemea.
Tulitoa wazo nyumba
tukaziangalia kwanza zile ambazo ni za kati walimu walipe shilingi elfu tano
lakini zile ambazo zipo kwenye mpango wa MEM na MES zilipiwe 10,000 na kwa zile
ambazohazifai kabisa wakae bure kwa sababu zipo katika hali nzuri.
‘’’’’ mtumishi wa
kawaida anaishi kwenye nyumba na kulipa shilingi elfu kumi na tano mpaka
ishirini lakini sisi tunatoza kiwango cha juu 10,000 hawawezi kushindwa
kulipia.’’’’ Alisisitiza Kongo
‘’’’’ ukiwa mtumishi
una mkataba wko ni suala la mwajiri kukupa motisha lakini kulingana na uwezo
hakuna mkataba wa kutoa nyumba bure huo ni mchangokwa mtumishi na halmashauri
ili tuweze kufanya ukarabati wa nyumba hizo.’’’’ Akaongeza kongo
Aidha mwenyekiti huyo
alimtaka afisa elimu msingi kuliangalia upya tangazo lililobandikwa katika ubao
wa matangazo likiwataka walimu kupeleka shida na matatizo yao siku ya ijumaa pekee.
Akaongeza kuwa
watumishi na watu wengine wanataka kupatiwa huduma mara zote na wakati wowote
sasa unapowapangia siku moja idadi ya watu zaidi ya mia mbili inageuka kero.
mwisho
No comments:
Post a Comment