Katika pitapita zangu leo nimebahatika
kupita barabara ya Matamba-Mfumbi ambapo nimekutana na mandhari hii
nzuri ya miti ya asili katika eneo hili lililopo tarafa ya Matamba
wilayani Makete na ukiangalia vizuri utaona maporomoko marefu ya maji
kwa mbali, ambayo yanazidi kuipendezesha wilaya ya Makete, kwa kweli inapendeza sana
wageni karibuni Makete na
pia wenyeji wa makete jijengeeni utaratibu wa kutembelea maeneo kama
haya ili kujionea mengi, maana utunzaji wa mazingira nao umechangia hali
hii ionekane
No comments:
Post a Comment