Watu wawali
wa wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya makete kujibu tuhuma za kugushi
sahihi na kuandika mhutasari katika kikao hewa na kuchukua zaidi ya shilingi
milioni mbili katika akaunti ya mfuko wa maendeleo wa kata ya bulongwa
Akitoa
taarifa hiyo kwa wanahabari ofisi kwa kwake mwendesha mashitaka wa PCCB bwana
Frednandi Nsakuzi amewataja watuhumiwa hao kuwa ni aliye kuwa diwani wa kata ya
Bulongwa Estomin Mahenge na mwenzake Edwin swallow ambaye alikuwa mtendaji wa
kijiji mpaka anafanya tukio hilo
alikuwa anakaimu ofisi ya mtendaji wa kata ya Bulongwa
watuhumiwa
hao waligushi sahihi na kuandika mhutasari wa kikao hewa na kwenda katika benki
ya Nmb na kuchukua zaidi ya shilingi million mbili kwenye akaunt ya mfuko wa
maendeleao ya kata ya Bulongwa wakidai kuwa ni kwajili ya ujenzi wa shule ya
sekondari Usililo ambapo mhutasari huo ulikuwa baadaye ya taasi ya kupambana na
Watuhumiwa
hao walifikishwa mahakamani hapo jana na walikana mashitaka yanayowakabili kesi
hiyo inatarajiwa kutaja tena tarehe 23
mwezi wa 3 mwaka huu katika mahakama wilaya makete
Aidha katika hatua nyingine mkurugenzi wa Pccb
wilayani Makete bwana Daudi Ndyamkama amewahasa wana makete kushilikiana na
taasisi hiyo pindi wanapokuwa na kesi kama hizo hususani inapokuwa katika hatua
ya ushaidi mahakamani bwana ndyamkama amesema kumekuwa na vitendo kama hivi
katika vijiji vingi wilayani hapa lakini wananchi wamekuwea hawatoi ushilikiano
katika kesi hizo pindi wanapo hitajika kutoa ushahidi mahakamani na badhi yao
wamekuwa wakirubuniwa na watuhumiwa
No comments:
Post a Comment