Na Denis Mlowe _- Iringa
Watoto wawili mapacha walioungana miili
yao Consolata na Maria Mwakikuti wenye miaka 15 wamelilia Waziri Mkuu
Mizengo Kayanza Pinda kutimiza ahadi yake aliyowapatia ya kuwapatia
umeme katika kituo cha Nyota Asubuhi kilichoko katika katika kata ya
Kidabaga Kijiji cha Ilamba Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa.
Walisema hayo baada ya kutembelewa na
mbunge wa viti maalum Ritta Kabati mwishoni mwa wiki na kueleza
kwamba tangu Waziri Mkuu atoe ahadi hajafika tena kijijini hapo na
umeme umekuwa ni kikwazo kwao kwani umeme wanaotumia wa solar na
jenereta haukidhi mahataji kwa kipindi hiki cha mvua hivyo kuna
wakati wanakosa umeme.
Watoto hao wenye uwezo mkubwa darasani
wakiwa kidato cha tatu katika shule ya sekondari ya Maria na
Consolata inayomilikiwa na kituo hicho ni wacheshi kama wakishakuzoea
lakini wenye aibu kama hawajakuzoea waliweza kueleza kuhusu maisha
yao na kuonyesha ni kiasi gani wanaimani kubwa na uongozi wa kituo
hicho wanapolelewa kwa kuweza kukiri kupewa huduma zote stahiki za
binadamu.
Mbunge Kabati aliwapowauliza awaletee
zawadi gani au msaada gani walisema wanapenda tu amfikishie ujumbe
Waziri Mkuu ahadi yake ya umeme na alipowaambia atawaletea simu na
komputa mpakato wakamjibu zote wanavyo shida yao kubwa ni umeme na
aliwaahidi kwamba atawafata waweze kwenda mapumziko sehemu
watakayopenda kwani wamekuwa watu wa chumbani, sebuleni na kanisani
nalo liko katika kituo hicho.
Mapacha hao wakiongea kwa furaha na
mbunge na waandishi wa habari waliowatembelea walionyesha kuwa na
furaha kutembelewa na kuwataka wananchi wenye uwezo wawatembelee na
kuwafariji na kusema wanashindwa kwenda nje ya hapo kwa kuwa watu
watawashangaa kutokana na hali yao ya ulemavu.
No comments:
Post a Comment