Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa kitendo hicho ni cha kinyama zaidi kutokea kufanyika katika eneo hilo na hii inaonesha jinsi gani watu wasivyo na utu.
"Inavyoonekana mtu huyu alijifungua halafu akamtupa mtoto huyu, hii ni ajabu sana kwa mtu kubeba mimba miezi tisa halafu kuamua kutupa kiumbe kisicho na hatia" alisema kijana huyo aliyefahamika kwa jina moja Rajabu
Kwa mujibu wa kijana aliyeona mwili huo alisema alikuwa anaelekea shambani na ndipo alipamua kupitia sehemu ambayo huwa anaficha jembe na kuona kiumbe huyo akiwa ametelekezwa huku akiwa amekwisha kufa.
"Inawezekana mtu huyu alimtupa mtoto huyu usiku kwani jana wakati naficha jembe hapakuwa na kitu chochote alisema kijana huyo.
No comments:
Post a Comment