MKAZI
wa jijini Dar es Salaam [mwanaume] jina lake halikuweza kupatikana mara
moja, amejikuta akishindwa kuendesha gari, baada ya kuporwa kompyuta
aina ya Laptop akiwa kwenye foleni katika barabara ya Nyerere |
Tukio
hilo lililoshuhudiwa na mwandishi wa habari hii jana majira ya jioni,
dereva huyo alijikuta akisababisha foleni baada ya taa kuruhusu na yeye
akijikuta akiduwaa mara baada ya kumtokea tukio hilo
Mkazi huyo
wa jiji alikuwa akiendesha gari ndogo aina ya Toyota huu mapajani mwake
akiwa ameweka Laptop hiyo kwa matumizi yake pindi alipokuta foleni
Kwa
kawaida majira ya jioni katika barabara nyingi jijini hususani hiyo ya
Nyerere hukabiliwa na foleni inayofanya kupatikana kwa kero kwa
watumiaji wake
Hivyo kutokana na foleni hiyo ambayo yeye aliiona
anaweza kufanya mambo yake mengine, akaamua kutumia komputa yake hiyo
akiwa kwenye foleni hiyo bila kutambua kuna wezi wanaotalii kuangalia
huko na kuko kwa anayezubaa ajinyakulie mali aina yoyote kwa abiria
wanaotumia daladala ama waliokuwa kwenye usafiri binafsi kisha kukimbia
Ghafla
foleni ilipokaribia kwenda akatokea kibaka mmoja kusogelea kwenye gari
hilo akamnyang’anya komputa hiyo na mmiliki huyo kubaki akiduwaa na
alipochukua uamuzi wa kumkimbiza hakuona hata vumbi lake
Huku
baadhi ya watu walioona tukio hilo waliokuwa kwenye foleni walimshauri
arudi garini kwa kuwa asingemuona tena mwizi wake huyo
Hivyo
muda wa kuruhusu magari kwa upande unaotokea mjini kuelekea maeneo ya
Uwanja wa Ndege ukawadia kutakiwa magari yapite kwenye foleni dereva
huyo alijikuta akisababisha foleni kwa kuduwaa licha ya madereva wenzake
kumuamuru aondoe gari hilo
Hata hivyo honi hazikuweza kuzaa
matunda hadi pale baadhi ya madereva walioshuka kumuamuru asonge mbele
kwa kuwa tayari foleni ilisharuhusiwa ndipo aliposonga mbele |
|
|
|
No comments:
Post a Comment