Saturday, December 15, 2012

WANAINCHI NJOMBE ARDHI BADO TATIZO

Wananchi wa Mitaa ya Ngalanga na Mji Mwema Mkoani Njombe Wameiomba Serikali Kusitisha Zoezi la Upimaji na Ugawaji Viwanja Kwenye Mitaa Hiyo Hadi Hapo Muafaka Utakapopatikana Baina Yao na Halmashauri ya Mji wa Njombe.

Aidha Wananchi Hao Pia Wamelalamikia Mwenendo Mzima wa Zoezi Hilo Kwa Kudai Kuwa Huenda Limegubikwa na Vitendo Vya Rushwa Kutokana na Baadhi ya Maamuzi Kufanywa Bila Kuwashirikisha Wananchi na Wamiliki wa Maeneo Husika.

Wakitoa Hoja Kumi na Moja Zinazohusu Muenendo Mzima wa Zoezi Hilo,Wananchi Hao Wamesema Kwanini Baadhi ya Maeneo Yamepimwa na Kuuzwa Bila Fidia Kwa Wahusika na Kuhoji Juu ya Uamuzi wa Serikali wa Kuwahamisha na Kuwasogeza Wamiliki wa Nyumba Pamoja na Kuwataka Kulipia Ardhi Yao Kwa Kiwango Ambacho Wamedai Hawakimudu

Aidha Miongoni Mwa Mambo Yaliolalamikiwa na Wananchi Hao Kuhusu Zoezi Hilo ni Pamoja na Viwanja Kugawanywa Kwa Kuchanganya Kati ya Majirani na Hivyo Kusababisha Ugomvi,Kutowekwa Wazi Kwa Ramani ya Mipango Miji ni Kiashiria Tosha Kuwa Zoezi Hilo Limetawaliwa na Rushwa Kwa Watu Wenye Uwezo Kupata Maeneo Mazuri.
 
Akizungumzia Hali Hiyo Afisa Ardhi Halmashauri ya Mji wa Njombe Bw Thadei Kabonge Amesema Kwa Sasa Hawawezi Kusitisha Zoezi Hilo Kwa Kuwa Tayari Wameshalipa Fidia Kwa Asilimia 64 Kati ya Wakazi wa Mitaa Hiyo

Mnamo Mwezi Nov Mwaka Huu Halmashauri ya Mji wa Njombe Ilitangaza Kuanza Zoezi la Upimaji na Ugawaji Viwanja Katika Maeneo ya Ngalanga na Mjimwema Ikiwa ni Mpango Mkakati wa Kuboresha Makazi na Upanuzi wa Mji Kulingana na Mahitaji na Maendeleo Yaliopo Kwa Sasa.

No comments:

Post a Comment