Naibu waziri wa maji na mbunge wa jimbo la Makete dk Binilithi Satano Mahenge akizingumza na wana nchi wa jimbo wananchi wilayani Makete hivi karibuni (picha na rizikimgyablogspot)
Naibu waziri wa maji na mbuge
wa jimbo la Makete DK Binilithi Mahenge ameahidi kuchangia shilingi milioni mbili katika mradi
wa umeme katika kijiji Ivalalila wilayani Makete mkoani Njombe.
Ahadi hiyo imetolewa mwishoni
mwa wiki hii mbele ya wanaichi wa Ivalalila akitoa ahadi hiyo Dk Mahenge alisema niwiwa na jitihada za wananchi kujitoa na
kuanzisha mradi huo wa umeme utokanao na maporomoko ya maji yaliyoko katika kijiji hicho.
Pia Mahenge aliwataka
wananchi hao kutokata tamaa na maendeleo ya kijiji hicho na kuahidi kuendelea
kukisaidia kijiji hicho na kwakushirikiana
na halimashauri ya wilaya “nitawaunga
mkono kwakushiriana na halmashauri ya wilaya kwa kupitia mfuko wa jimbo ili
kuwaunga mkono kwa jitihada za maendeleo nimefurahishwa sana na uwajibikaji
wenu hii inatia moyo pia natoa rai yangu kwa wananchi wa sehemu nyingine waige
mfano huu ili kujikwamua na umasikini” alisema Dk Mahenge.
Awali Dk mahenge alifanya ziara yake katika
kijiji cha Ndulamo kilichopo wilaya hapa na kuzungumza na wananchi wa kijiji hicho
ambopo walitoa kero zao mbele ya naibu wa maji ambaye pia ni mbuge wa
jimbo hilo huku kero ya maji ikiwagusa sana wananchi wakiji hicho na wakalazimika kumueleza
Dk Mahenge kilio cha maji kilichopo kijijini
hapo kuwa imekuwa ni moja kati ya vitu vinavyo changia kushuka kwa maendeleo
kijijini hapo “tunateseka na adha ya maji tunaomba kama mbuge wetu ambaye
unasikiliza vilio vya wanachi wako na kwa kuwa ni naibu waziri wa maji
tusaidie”walisema wanakijiji hao.
Kwaupande wake diwani wa kata
ya iwawa ndugu Alibaha Mahenge kero zipo nyingi ila kwa kusaidina na
halimashauri pamoja na mbuge watazitatua.
Dk Mahenge yupo wilayani Makete kwa zira ya
siku tatu ziara hiyo imeamilizika kwa kutembele katika kata za
Matamba,Kipangalo,na Iwawa .
No comments:
Post a Comment