Na Prince Akbar
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo asubuhi imemuachia kwa dhamana msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu, anayetuhumiwa kumuua msanii mwenzake, Steven Kanumba ‘The Great’ baada ya kupitia vifungu vya sheria.
Hatua
hiyo inakuja baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kubadilisha
mashitaka ya mwanadada huyo kutoka kesi ya mauaji hadi kuua bila
kukusudia.
Kutokana
na mabadiliko hayo, hata kama atashindwa kesi, Lulu hatapewa hukumu ya
kunyongwa kwa kuwa anatuhumiwa kwa kesi ya kuua bila kukusudia na kwa
mujibu wa kifungu cha sheria, anaweza kufungwa maisha au miaka kadhaa.
Lulu anakabiliwa na tuhuma za kumuua The Great Kanumba aliyefariki dunia, Aprili 7, mwaka huu nyumbani kwake Vatican, Sinza Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment