Hadza
au Wahadzabe ni kabila linaloishi katika kaskazini ya kati Tanzania
wanoishi kuzunguka ziwa Eyasi katikati ya bonde la ufa na eneo la jirani
ya serengeti na hapa ni vijana wakicheza ngoma za kitamaduni.
Hadza
ni kabila lenye idadi ya watu wasiozidi 1000 na hapa ni binti wa kabila
la hadza akicheza zeze ya kiasili.hii inaonyesha ni jinsi gani muziki
siyo teknolojia.
Wanatofautiana
na watu wa kawaida kijenetikia na jadi yao ni ya lugha ya Khoisan
inayoonekana kujijenga na kutohusiana na watu wengine
Baadhi ya mapambo ya kitamaduni na fuvu za wanyama kutokana na kabila hili kuishi kwa kutegemea uwindaji kwa kiasi kikubwa.
Karibu
kuwatemelea Wahadzabe na ujue kuusu utamaduni wao.Tunaweza kuandaa
safari za kutembelea makabila mbalimbali kutokana na vile unavyotarajia
kujifunza na kukuza utalii wa ndani na nje pia.Karibu Arusha weka maoni
yako kwa unachotaka kujua kuusu kuwatembelea.
Wahadzabe
wana maeneo manne ya makazi kame kusini mwa Ziwa Eyasi na kati ya ziwa
Eyasi na Bonde la Yaeda mashariki katika nyanda za juu Mbulu( Siponga)
na kaskazini mwa bonde karibu na mji wa Mang"ola.
Wakati
wa msimu wa mvua Hadzabe hutoka nje kati ya maeneo haya na usafiri
kiurahisi msimu wa kiangazi na hii ni nyumba ya kuishi inayotumika na
kabila la Wahadzabe
Kabila
hili linaishi kwa kutegemea uwindaji wa wanyama kwa kiasi kikubwa na
chakula chao kikuu ni nyama ambayo huifadhiwa kwa kuanikwa juani kwenye
miti.Pichani ni baadhi ya wanyama pori aina ya swala ambao Hadza
huwawinda kwa wingi
Pia
wanishi kifamilia na hapa na wakina mama na watoto wa kabila la
Hadza.Rika la vijana huwa wanawinda na chakula kuliwa na wote
Matumizi
ya tumbaku na bangi na moja ya starehe ya vijna wengi wa kabila la
Wahadzabe na kuwasha moto huwa wanatumia kijiti kikavu, magome ya mti
kupekecha hadi moto kuwaka na kutumika kwa matumizi mbalimbali na Hadza
300 hadi 400 hishi kwa kiasi kikubwa kwa uwindaji kama babu zao. KARIBU
ARUSHA.
No comments:
Post a Comment