TUME ya Utangazaji Zanzibar
(TUZ) imesimamisha matangazo yote yanayohusiana na vurugu zinazofanywa na watu
wanaosadikiwa kuwa wafuasi wa Uamsho Zanzibar.Kwa mujibu wa barua ya Tume hiyo
kwa vyombo vyote vya habari, radio na Televisheni marufuku kutangaza matukio
hayo na kituo chochote kitakachokwenda kinyume hatua za kisheria zitachukukuiwa
dhidi yake.
“Kutokana na kukabiliwa na machafuko ndani ya nchi kumejitokeza baadhi ya vikundi vya watu wanaojiita uamsho na kusababisha vurugu ndani ya nchi Tume inasitisha matangazo yote yanayohusiana na vurugu hizo,” imeeleza sehemu ya barua iliyotolewa jana.
Barua hiyo yenye kumbukumbu namba TUZ/ SGL2/VOL.2/ 42 imesainiwa na Mtumwa B Mzee kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa Tume hiyo na kusabazwa kwa vituo vya radio na televisheni visiwani humo.
“Kituo chochote kitakachokwenda kinyume na agizo hili bila ya idhini ya Tume ya Utangazaji Zanzibar hatua zinazofaa zitachukuuiwa dhidi yake,” imesisitiza barua hiyo yenye kichwa cha habari ,“Kusitisha matangazo ya vipindi vya Uamsho”.

No comments:
Post a Comment