TAASISI ya Masheikh na Wanazuoni wa Kiislam Tanzania imewaasa Watanzania kuzingatia utawala wa sheria na kutii amri za mamlaka zilizoundwa kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Taasisi hiyo, Sheikh Khamis Mataka, alisema kuwa wamelazimika kutoa kauli hiyo kutokana na baadhi ya Waislamu kuwa na ghadhabu na kusababisha uharibifu wa mali za watu wasio na hatia na kuchoma makanisa.
Alisema taasisi hiyo ilifanya mkutano kwa siku mbili kutafakari afya ya jamii kufuatia tukio la kunajisiwa kwa Kuran Tukufu na ghasia zilizotokea Mbagala zilizohusisha kutotii sheria na amri za mamlaka na uchomaji wa makanisa.
Sheikh Mataka aliongeza kuwa sekretarieti yao imetazama suala la vurugu zilizotokea Kariakoo ambapo baadhi ya waumini waliishia mikononi mwa vyombo vya dola na pia waliangalia vurugu za Zanzibar ndipo wakatoa tamko hilo.
Alisema taasisi hiyo imesikitishwa sana na baadhi ya Wasilamu kutumia mikusanyiko isiyo halali kupingana na Jeshi la Polisi chini ya shinikizo la kutaka kuachiwa watuhumiwa waliokuwa wamekamatwa.
Mataka alisema kinachofanyika sasa ni watu kutozingatia mafundisho ya dini kwani yanahimiza utulivu, amani na kuheshimu kila kilichowekwa kwa taratibu na kuwataka viongozi wote wanaohamasisha machafuko kurejea mafunzo hayo kama msingi wa kudumisha amani nchini.
Alibainisha kuwa taasisi hiyo imeshtushwa na baadhi ya matamko ya viongozi wa dini ya Kikristo yanayotaka kuitumia kadhia hii kuutia doa Uislamu na Waislamu na kujenga uhalali wa kuitikisa misingi ya udugu kiasi cha kutamani kuzaliwa Tanzania mpya.
Sheikh Mataka alisisitiza kuwa kauli ya maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) iliyotolewa hivi karibuni ilikuwa na mafumbo na hivyo kuzua hofu.
Hata hivyo alisema kuwa taasisi hiyo imesikitishwa na baadhi ya askari waliotumia vibaya ruhusa ya kutumia nguvu katika kuzima fujo hizo, bila kuzingatia mazingira na maeneo yenye mikusanyiko mikubwa ya watu na shughuli za kiuchumi.
“Taasisi pia inatoa pole kwa Rais wa Zanzibar na Mkuu wa Jeshi la Polisi kufuatia kuuawa kinyama kwa askari asiye na hatia, Saidi Abdulrahman na pia kutokana na vurugu hizo tunatarajia kuitisha kikao cha masheikh na viongozi wa taasisi mbalimbali za Kiislamu ili kutafuta dawa ya tatizo hili,” alisema Mataka.
Aliongeza kuwa mbali na kuitisha kikao cha viongozi wa Kiislamu lakini pia taasisi inatarajia kuitisha kikao cha viongozi wa dini mbalimbali ili kujadili miundo bora ya kudumisha amani, utulivu na uhusiano mwema baina ya wanadini kwa misingi ya kila mmoja kumheshimu mwenzake.
Taasisi hiyo pia iliwatahadharisha wanasiasa kujiepusha kwa namna moja au nyingine kubariki vurugu za vikundi vya kidini na jamii kwa ujumla na ikawataka waache kutoa ushawishi wa kujichukulia sheria mikononi na kuhamasisha kutotii amri halali za mamlaka za nchi.
Akijibu swali la waandishi waliotaka kujua endapo angekutana na Sheikh Ponda leo atamshauri nini, alisema atamwambia azingatie Uislamu katika kufanya mambo yake.

No comments:
Post a Comment