Sunday, October 14, 2012

RC NJOMBE AWASASUSA WANAHABARI MAKETE


Mkuu wa mko Njombe Aser Msangi (picha kwa msaada wa mtandao)

Katika hali isiyo yakawaida  Mkuu wa mkoa wa Njombe Aser Msangi  mwanzoni mwa wiki hii alifanya ziara ya siku moja katika wilaya ya makete bila ya waandishi wa habari  nakutembelea baadhi ya maeneo ikiwamo kata ya Ipelele tarafa ya Magoma.

     Kutoka katika chanzo chetu cha kuaminika mkuu huyo wa mkoa alifanya ziara hiyo bila ya kuongozana na mwandishi yoyote wa  chombo chochote ndani na nje ya mkoa huu.

      chanzo chetu kimeueleza mtandao huu kua mkuu wa mkoa akiwa  ameongozana na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Makete walifika katika kata ya Ipelele kuaajili ya kukabidhi hundi ya shi milioni tatu kama ahadi ya Mh Jakaya kikwete alizoahidi kutoa katika shule ya secondary Ipelele kusaidia ujenzi wa shule hiyo
akikadhi hundi hiyo Mkuu huyo wa mkoa aliwaeleza wanachi wa wa kata hiyo kuongeza juhudi wa katika kilimo ili kufikia mapinduzi ya kijani ili kufikia malengo ya millenia .

         Licha ya mkuu huyo kutoongozana na mwandishi yoyote lakini mtandao huu ilifanya mahojiano na baadhi ya wananchi wa maeneo ambako mkuu huyo alifanya ziara hiyo wameoneka kusikitishwa na kitendo hicho na kusema licha ya kuwapo na redio katika halimashauri ya wilaya hiyo rakini hakuna mwandishi aliye alikwa katika ziala hiyo kitu ambacho kinawanyima frusa wananchi kujua habari ndani ya wilaya yao.
 

No comments:

Post a Comment