PASUA KICHWA YA JAMII YETU TANZANIA GROUP LEO
Jamaa mmoja alikuwa ni bingwa wa kutongoza wake za watu ,na mkewe alipata hizo habari kutoa kwa watu ila hakuziamini siku moja aliamua kufanya uchunguzi wake aliamua kuvaa nguo za rafiki yake ambaye pia ana ndoa yake na kutoka kwenda kusimama katika eneo lenye giza ambapo mume wake huyo amekuwa akipita mara kwa mara haikuchukua muda jamaa mpenda wake za watu akatokeza eneo hilo na kama kawaida alianza kumtongoza mwanamke huyo asijue ni mke wake na kumumwagia sifa nyingi na baada ya hapo mwanamke huyo ambaye ni mke wake alikubali na kutaka kupewa kabisa fedha yake kiasi cha Tsh.50,000 ,kama kawa jamaa alitoa na kuanza safari ila cha kushangaza mwanamke huyo aliongoza njia na kuelekea maeneo ya kwake huku akijifunia ushungi usoni na ghafla alimgeukia na kumuuliza wataka twende wapi ?jamaa kuona sura ya mke wake alianguka na kupoteza kuzimia kwa hofu ,Je ? ungekuwa wewe ungefanyaje?
|
No comments:
Post a Comment