Vicky Macha (kushoto) enzi ya uhai wake akiwa Anita Boma wakati wakienda Ruaha National Park mwezi Mei mwaka huu.
Mweka Hazina wa Klabu ya Waandishi wa
Habari Iringa (IPC), Vicky Macha, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo
baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Taratibu za mazishi zinafanywa.
Ndugu wanakijiji wenzangu, tuungane kwa pamoja katika kuomboleza msiba
huu mzito uliowapata wenzetu wa IPC katika kipindi cha takriban mwezi
mmoja tu tangu kuondokewa ghafla na Mwenyekiti wao, marehemu Daudi
Mwangosi.
Tutaendelea kujulishana taarifa mbalimbali za msiba huo.
No comments:
Post a Comment