UCHAGUZI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi
(UVCCM), umemalizika mjini Dodoma huku ukigubikwa na vituko vya kila
aina ikiwemo naibu mawaziri wawili kudaiwa kugawa rushwa.
Sakata hilo linakuja ikiwa ni muda mfupi tangu mkuu wao, Rais Jakaya Kikwete, afungue mkutano huo na kuonya vikali dhidi ya vitendo vya rushwa ndani ya chama, huku akiwataka vijana hao kusimama kidete.
Naibu mawaziri hao ambao majina yao tunayahifadhi, wanadaiwa kuzusha tafrani kubwa nje ya ukumbi wa uchaguzi huo juzi, pale walipobainika wakitembeza rushwa hadharani kwa wajumbe.
Inadaiwa kuwa hali hiyo iliibua mzozo mkali baada ya baadhi ya wajumbe kumweleza jambo hilo mmoja wa viongozi wa UVCCM wanaomaliza muda wao, ambaye alikwenda mbio eneo hilo na kuwataka vigogo hao waondoke mara moja.
Tanzania Daima ilidokezwa kuwa vigogo hao wa Serikali ya Kikwete, walikuwa wakimuunga mkono mmoja wa wagombea nafasi ya umakamu mwenyekiti wa UVCCM ambaye hata hivyo alishindwa.
Mmoja wao alipotafutwa na gazeti hili jana mchana, licha ya kukiri kufika eneo la mkutano, lakini alikanusha tuhuma hizo akisema ni uzushi wa kutaka kumchafua.
“Mimi nimefika kwenye mkutano huo na kweli nilikuwa namuunga mkono mmoja wa wagombea kama walivyokuwa wakifanya wenzetu, lakini tulifanya kampeni zetu bila kutoa hata shilingi, sasa hayo madai nasikia kwako na si kweli,” alisema naibu waziri huyo.
Katika uchaguzi huo ambao umemleta madarakani Mbunge wa Donge, Sadifa Juma Khamis, kama mwenyekiti mpya wa UVCCM na Makamu wake Mboni Mhita, ulidaiwa kutawaliwa na vitendo vya rushwa iliyokuwa ikitolewa wazi wazi kwa wajumbe.
Akitangaza matokeo hayo jana, msimamizi mkuu wa uchaguzi huo, William Lukuvi, alisema kuwa Sadifa alipata kura 443 na kumbwaga mpinzani wake, Rashid Simai Msarika aliyepata kura 267.
Wagombea wa nafasi hiyo walikuwa watatu wote kutoka Zanzibar, lakini Lulu Msham Abdalla, alijitoa kwa kuwa aliteuliwa kugombea nafasi nyingine ya ujumbe wa Baraza Kuu viti vinne Zanzibar.
Mboni alijikusanyia kura 489 katika nafasi ya makamu mwenyekiti na kumgalagaza kada maarufu, Paul Makonda, aliyepata kura 241 na hivyo kuibua malumbano makali baina ya wafuasi wao.
Hata hivyo, uchaguzi huo ulitawaliwa na makundi ya wagombea urais mwaka 2015 jambo lililosababisha pande zote kutuhumiana kwa rushwa.
Kufuatia sintofahamu hiyo ya tuhuma za rushwa, baadhi ya wajumbe walimpa saa 24 Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Kikwete, wakimtaka atengue matokeo hayo kutokana na kugubikwa na tuhuma hizo.
Wajumbe hao waliwatuhumu wazi wazi viongozi wa kitaifa waliomaliza muda wao, yaani Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM, Hussein Bashe, Kaimu Mwenyekiti, Benno Malisa na Katibu Mkuu, Martin Sigela kuwa waligawa rushwa kama njugu.
Viongozi hao walidaiwa kuwapigia kampeni baadhi ya wagombea, hasa Mboni.
“Kaimu Mwenyekiti na Katibu Mkuu walivunja kanuni za uchaguzi kwa kuwapigia kampeni baadhi ya wagombea, ikiwa ni pamoja na kugawa rushwa kama njugu ili watu wao wanaowataka washinde,” alidai mmoja wa wajumbe hao.
Walidai kuwa wana ushahidi wa kutosha wa picha za viongozi hao wakiwagawia makatibu rushwa ya sh milioni moja kila mtu, ambazo zilikuwa zikigawiwa chooni.
“Wakati uchaguzi ukiendelea jana, viongozi hawa walikuwa hawakai jukwaani na badala yake muda wote walikuwa nje na kumfanya msimamizi mkuu wa uchaguzi kupaza sauti ya kuwaita ukumbini mara kwa mara,” alisema mjumbe mmoja.
Itakumbukwa kuwa muda m
fupi kabla, Rais Kikwete alifungua mkutano huo wa vijana na kuwaonya kujiepusha na vitendo vya rushwa na kutumiwa na watu wanaosaka urais.
Wajumbe hao walidai kuwa kama Mboni angeshinda katika utaratibu unaokubalika, wasingekuwa na tatizo. Kwamba wanachokilalamikia ni uchaguzi huo kutokuwa wa haki.
Kwamba uchaguzi huo ulivamiwa na watu wasiohusika ambao walikuwa nje wakiwaita baadhi ya wajumbe na viongozi kuzungumza nao huku wakiwagawia fedha.
Kivimba Suleimani ambaye alikuwa mgombea ujumbe wa Baraza Kuu la UVCCM, alisema kwa hali halisi ya uchaguzi ilivyokuwa, ni vigumu kwa mtoto wa masikini kushinda.
Alitoa wito kwa wajumbe wenzake na kuwataka wabadilike kwani fedha wanazopewa kiasi cha sh 50,000 hadi 100,000 zinapita, lakini Tanzania itabaki palepale.
Naye mjumbe mwingine, Kichanta Damiani, alisema baada ya rais kufungua mkutano huo, uchaguzi uliendelea vizuri, lakini baadae viongozi walianza kutoka mmoja mmoja kwenda kuwapigia wagombea wao kampeni.
“Natolea mfano Benn
o, muda wote alikuwa nje na kuna kipindi alisimama nyuma ya msimamizi wa uchaguzi akiwafanyia ishara wajumbe, akimaanisha kama vile kazi imemalizika.
“Baada ya hali hiyo mimi niliamua kwenda kwa Lukuvi nikamueleza, akaniambia nashukuru kwa taarifa, ndipo akamuita Benno akae kwenye kiti chake, lakini hata hivyo alikuwa akitoka nje mara kwa mara,” alisema.
Hata hivyo, nusura vurugu itokee kwani wakati wajumbe hao wakilalamika kwa waandishi wa habari, wengine kutoka Arusha walivamia mazungumzo hayo wakikanusha madai yake.
Katibu Mwenezi wa Wilaya ya Mbuguni, Joshua Mbweni, aliwataka wanaokataa matokeo wakubali kushindwa kwa kuwa uchaguzi ulikuwa wa haki.
Mjumbe mwingine alidai kuwa tatizo lilikuja pale wagombea waliowekwa na watoto wa vigogo waliposhindwa ndipo baadhi ya wajumbe hao wakaanza kuyapinga matokeo.
Wakati hayo yakiendelea, Bashe alikutana na waandishi wa habari na kukanusha tuhuma dhidi yake kuwa anatumiwa na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, ili kumwaga fedha kwa wajumbe kumuwezesha Mboni kushinda.
Bashe alisema kuwa yeye hatumiwi na Lowassa na wala hafanyi kazi zake binafsi, bali anafanya kazi ya kukitumikia chama chake cha CCM.
Alisema hayo wanayoyasema si sahihi kabisa bali ingekuwa sahihi kama wangesema yeye anamtumaini Lowassa kutokana na uvumilivu wake licha ya kukumbana na mikiki mingi ya kisiasa, lakini ameendelea kuwa shupavu na imara katika chama.
“Mimi namtumaini Lowassa na ninajifunza mambo mengi sana kutoka kwake kwani ni moja kati ya wanasiasa nchini ambao wamekumbana na mambo mengi, ikiwa ni pamoja na kutuhumiwa, kusemwa na kuchafuliwa, lakini hajatetereka na ameendelea kukitumikia chama chake,” alisema Bashe.
Aliwataka wanaomtuhumu kama wana ushahidi wa kutosha wapeleke Takukuru pamoja na kwenye uongozi wa chama ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake.
Askari atumbukia UVCCM
Askari namba F 7961 PC Stanley Mdoe, anayefanya kazi katika kituo cha polisi Mvomero mkoani Morogoro, anadaiwa kujihusisha na siasa kwa kuingia kwenye kugombea ujumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) Taifa kupitia kundi la vijana.
Chanzo chetu kilieleza kuwa, askari huyo anayejitambulisha kama mtoto wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, akijitambulisha kwa jina la Stanley Bendera, alikamatwa mkoani Dodoma juzi jioni wakati uchaguzi wa UVCCM ukiendelea.
Kwamba akiwa amevalia sare za chama hicho tangu siku ya kwanza akiomba kura kwa wajumbe, huku akiwa amepamba gari yake kwa picha zake, baadhi ya wanachama wanaomfahamu waliwatonya maafisa usalama waliokuwepo eneo hilo.
Tanzania Daima ilitonywa kuwa maafisa hao nao walitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi mkoani Dodoma ndipo alipotiwa mbaroni.
Aidha, askari huyo pamoja na juhudi zake za kusaka ujumbe wa NEC, lakini hakushinda.
Kumekuwa na mkanganyiko kuwa askari huyo tayari aliomba likizo isiyokuwa na malipo, lakini taarifa nyingine zinasema aliacha kazi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, alisema kuwa hana taarifa ya askari huyo kujihusisha na masuala ya kisiasa.
Shilogile alisema kuwa alipata taarifa za kukamatwa kwa askari huyo mkoani Dodoma, na kwamba yeye alikuwa akimtafuta kwa shughuli za kikazi kwa muda wa siku mbili bila kumpata.

No comments:
Post a Comment