UKITAKA kujua tabia ya mtoto anza kufuatilia tabia ya wazazi
wake na hapo ndipo unapoweza kugundua kuwa mtoto mwizi lazima atakuwa
ameiga kwa mmoja wa wazazi wake na pengine hufanya hivyo bila kujua kuwa
wizi ni kosa.
Ukiona mtoto ana tabia ya kugombana kila siku na wenzake anapocheza nao, lazima ujiulize kuwa kwa vyovyote atakuwa ameiga kutoka kwa wazazi wake ambao hawawezi kupata usingizi bila kugombana na mara nyingi ugomvi huanza kabla ya chakula cha usiku na watoto hawajalala.
Ukiona mtoto anapenda sana kutukana na kuwa bingwa wa kutoa lugha chafu, lazima ujue kuwa darasa la kwanza la aina hiyo limeanzia kwa wazazi wake. Lazima mmoja wao ni bingwa wa kutoa lugha chafu kiasi cha kufanya ajulikane hivyo mtaani.
Ukiona mtoto kila anapoulizwa na watu wazima mara zote anajibu majibu ya uongo, lazima ujue sehemu kubwa ya uongo huo amefundishwa na wazazi wake ambao wanaona fahari kubwa kuijenga familia yao iwe ya watu waongo tu. Uongo wa faida na hasara kwao ni sawa.
Naweza kusema tabia hizo sio nzuri kwa malezi ya watoto na kwa vyovyote vile mtu akizizoea ndani ya familia na baadae hutoka nje. Tabia mbaya zikitoka nje huongeza maarifa zaidi na kurudi tena ndani.
Tabia mbaya kwa kawaida zikitoka ndani, zikaenda nje na kurudi tena, hapo zinakuwa mbaya zaidi na haziwezi tena kupatiwa dawa. Kwa kuwa mtu aliyeamua kuwa mwizi kuanzia ndani ya familia yake akatoka nje, huyo sasa ni mwizi sugu.
Ukiona mtu mgomvi hujue kaanzia ndani ya familia yake na baadae kaingia mitaani. Mtu huyo ataendelea kuwa mgomvi kwa mazoea na anaweza kuingilia ugomvi wowote bila hata kujua kiini cha tatizo na hiyo ndiyo tabia ambayo wengi wanajiuliza hadi leo kuwa hawa wanaogombana ugomvi wao una asili gani?
Najaribu kuweka taswira yangu na mtazamo wangu kuhusu mambo haya ya aibu yanayoendelea kukivua nguo Chama Cha Mapinduzi (CCM) na jumuiya zake ambazo kwa namna moja zinaweza kukisaidia chama hicho, lakini kwa upande mwingine zinakiangamiza.
Haitoshi kwa Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete, akemee tu tukio moja kubwa linalokitikisa chama hicho, vitendo vya rushwa kuwa ni kikwazo kikubwa mno cha kuweza kuwapata viongozi waadilifu ndani ya chama hicho.
Rushwa ni chimbuko la mzazi mwizi ambaye ameamua kumfundisha mtoto wake kuiba, na kwa vile binadamu ameumbwa na tabia ya kusahau, inakuwa vigumu kukumbuka kuwa wakati baba akiiba au mama akiiba mtoto wao alikuwa akijifunza tabia hiyo ya wazazi wake.
Kwa maana hiyo rushwa ndani ya chaguzi za CCM na jumuiya zake sio mchezo ulioweza kuibuka leo hii, ni matokeo ya muda mrefu na malezi mabaya ambayo kimfumo yameweza kujengwa ndani ya chama hicho na kwa kuwa tatizo hilo limekwisha kuwa sugu, si rahisi likaondoka ndani ya CCM.
Matukio ya wagombea wa nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho kupigana, kutishiana silaha, kutukanana, kutupiana vijembe vya karaha na aibu na kutoa matusi ya nguoni hadharani kunatokana na hali iliyofikia ukomo ya watu kushindwa kuvumiliana, kuheshimiana na kila mmoja kuwa tayari kuuza utu wake kwa ajili ya nafsi ya mwingine.
Matendo hayo yote ni dalili za wazi kuwa watu wa familia moja ukiona wameanza kutafutana uchawi ujue mwisho wa kuishi pamoja umetimia na dalili zinaonyesha wazi kuwa mwisho wa CCM kuishi na jumuiya zake umetimia.
Haiwezekani mwenyekiti wao akemee rushwa ndani ya chaguzi za jumuiya hizo, kisha wale wanaoambiwa waache rushwa wanambeza na kugeuza mfumo wa kupeana rushwa kwa njia ya mtandao, wanashindwa kuheshimu kauli ya mwenyekiti wao ya kuwataka waache rushwa.
Amewaambia wafanye kampeni za kistaarabu, hawataki wanafanya kampeni za makundi yanayoongozwa na uhasama mkubwa kiasi cha kuwafanya wengine washikane mashati na hao wote baba yao ni mmoja na mama yao ni mmoja, ukiona hivyo ujue wazi kuwa familia hiyo lazima isambaratike.
Nimeamua leo niseme haya na hasa nataka kuisema Jumuiya ya Wanawake ya CCM (UWT). Kwa mawazo ya wanawake wengi wamekuwa wakiamini kuwa jumuiya hiyo ni taasisi ya serikali kwamba ni chombo cha kuwaunganisha wanawake wote Tanzania, kumbe hali haiko hivyo.
Wanawake wengi walikuwa na mtazamo huo, kuwa Jumuiya ya Wanawake wa Tanzania kwa tafsiri nyingine ya kichama kuwa ni Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ulikuwa umebeba taswira zaidi ya wanawake wote wakati wa mfumo wa chama kimoja cha siasa na wengi hawakuwahi kufikiria mapema kuwa baada ya mfumo wa vyama vingi vya siasa, UWT ni mali ya CCM.
Ndiyo maana hivi sasa kila chama cha siasa kina vitengo vyake vya kuvisaidia vyama hivyo, vitengo hivyo au jumuiya hizo si vyama vya siasa, havijasajiliwa kuwa vyama vya siasa isipokuwa ni viungo vya chama cha siasa kilichosajiliwa na huo ndio ukweli, hakuna chama cha siasa kinachoitwa UWT.
Kwa mazingira hayo matukio yote mabaya ya kutoa rushwa na kupokea rushwa yanayofanywa na jumuiya za chama fulani yanakichafua chama hicho kwa kuwa vitendo hivyo vinatafsiri malezi halisi ya watoto waliyopata kutoka kwa wazazi wao.
Ndiyo maana nasema hivi, ukiona UWT wanatukanana hadharani na kutaka kugombana, lazima kwanza ujiulize baba yao na mama yao ni nani, ukiona UVCCM wanatuhumiwa kupenyeza rushwa na kugawanyika katika makundi ya wanamtandao, lazima ujiulize wazazi wa vijana hao ni nani, na ukiona Jumuiya ya Wazazi nao hawaelewani basi lazima ujue kuwa familia hiyo imefikia ukomo.
Ni aibu kuona kinamama wakirushiana maneno makali na yasiyokuwa na kiwango cha kuyachuja mbele ya hadhara tu kwa sababu, huyu ni waziri na huyu ni mbunge ambao wote wamezaliwa na kulelewa ndani ya chama hicho. Ukiona hayo yanatokea lazima ujue mwisho na mustakabali wa jumuiya hiyo si ushindi tena, ni mzigo ndani ya chama.
Kwa magomvi haya, kwa aibu
ya rushwa, kwa vitendo vya kibabe na kutishana, kwa vyovyote vile kumeanzisha safari mbaya ya kuelekea mwaka 2015 kwa kuwa hawa walioamua kugombana leo kwa ajili ya fedha za rushwa, hawawezi tena kuwa marafiki ili wajipange kugombana na adui wao wa kisiasa mwaka 2015.
Rais Kikwete ana kazi kubwa ya kukijenga chama chake, anaamini kuwa CCM haiwezi kufa, lakini kufa kwa chama hicho maana yake ni kupoteza dola, kilichokuwa chama kikuu cha siasa nchini Kenya, KANU hakijafa, lakini kimekufa kwa kuwa kimepoteza dola, kufa kwa chama tawala ni kupoteza dola.
Dalili zinazoendelea kutokea ndani ya chaguzi za chama hicho si za ushindi, si za kuilinda dola, ni dalili tosha zinazoonyesha kuwa CCM inaelekea mwanzo wa mwisho wa harakati zake za kujizuia kufa kwa kuwa watakaoweza kuiua ni watoto wake, ni jumuiya zake ambako huko ndiko chimbuko kubwa la rushwa ambayo rais anaomba Watanzania wamtajie wala rushwa.
Kama rais anafahamu kuwa rushwa imeota mizizi ndani ya CCM na jumuiya zake, iweje Watanzania wengine wasiokuwa wana CCM wafanye kazi ya kuwataja wala rushwa wakati anajua wazi kuwa hata Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye amesema rushwa ya mtandaoni itaimaliza CCM?
Ndiyo maana nasema haya yanayotokea UWT yanaweza kuwa chimbuko la ushindi wa chama hicho mwaka 2015.
“Ukiona kiongozi anawagawanya watu kwenye makundi hafai, ukiona kiongozi anaulizwa maswali anaamua kugombana, huyo hatoshi kwenye uongozi na ukiona kiongozi amepatikana kwa rushwa si mwenzenu,” alisema Rais Kikwete akifunga mkutano mkuu wa UWT, mjini Dodoma.

cnyenyembe@yahoo.com 0754 301864, 0715 301864
KWA MSAADA NA TANZANIA DAIMA
No comments:
Post a Comment