Watu 12
wanashikiliwa na polisi wilayani Mpanda mkoani Katavi kwa tuhuma za
kuteka basi la la kampuni ya Sumry mwishoni mwa wiki.
Watuhumiwa hao wanadaiwa kuteka basi lenye namba za usajili T 902 AZT
Nissan Diesel ambalo lilikuwa likiendeshwa na na Khalid Makamba
Oktoba 17 saa 6:23 usiku katika eneo la Magamba lililopo katika Tarafa
ya Nsimbo wilaya ya Mlele.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Joseph Myovela, alisema watekaji
wakiwa na marungu, mapanga na nondo waliweka mawe barabarani na
kufanikiwa kuteka basi hilo lilikuwa na abiria wakitokea Sumbawanga
kuelekea wilayani Mpanda.
Majambazi hao walipora abiria simu, pesa na vitu mbalimbali ambavyo thamani yake bado haijajulikana.
Aliwataja watu hao kuwa ni Elias Zakaria (45), mkazi Katumba na Mbuya
Michael (25) na Moses Liberatus (24), wakazi wa mjini Mpanda; Jackson
Lucas (27), mkazi wa kijiji cha Katisunga wilayani Mlele; Mussa Nassor
(17) na Ramadhani Hassan (17) ambao ni wakazi wa mtaa wa Majengo
wilayani Mpanda.
Wengine ni wakazi wa Majengo Abdallah Hassani (19), Joseph Masesa (22),
Sayo Masunga (18), Christopher Kwebe (20), Elias George (24) na
Shaban Loxagune (22), mkazi wa makazi ya wakimbizi ya Katumba Wilaya ya
Mlele.
Alisema upelelezi utakapo kamilika watafikishwa mahakamani kujibu mashitaka.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment