Rais wa Marekani Donald Trump amemfuta kazi
kaimu mwanasheria mkuu Sally Yates saa
chache tu baada ya kuwaagiza mawakili wa
idara ya haki nchini humo kutotetea uamuzi wa
kuwawekea vikwazo raia wanaotoka katika
baadhi ya mataifa ya kiislamu.
Taarifa ya Ikulu ya Whitehouse imemshtumu
kwa usaliti.
Sally Yates ambaye aliteuliwa na Obama
alisema kuwa hafikirii kwamba marufuku hiyo
ya muda kwa raia wa mataifa saba ya Kiislamu
ni halali.
Wadhfa wake umechukuliwa na kiongozi wa
mashtaka katika mahakama ya kijimbo huko
Virginia Dana Boente.
Agizo hilo la rais lililotiwa saini Ijumaa iliopita
limesababisha maandamano nchini Marekani na
ughaibuni.
Awali kundi moja la wanadiplomasia liliandika
barua likikosoa agizo hilo wakisema litazidi
kuhatarisha usalama wa taifa hilo.
Monday, January 30, 2017
Huyu Ndiye Trump Bana.. Amtimua Kazi Mwanasheria Mkuu wa Serikali Baada ya Kupinga Mpango Wake wa Kuwazuia Waislamu Wasiingie Marekani..!!!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment