Monday, May 16, 2016

Sheria ya mitandao ina lengo jema-Jaji Othman


Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohammed Chande Othman, amesema sheria ya mitandao ilipitishwa kwa lengo jema la kulinda watumiaji, wanajamii na usalama wa Taifa la Tanzania.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohammed Chande Othman.
Ametoa kauli hiyo wakati akijibu baadhi ya maswali kutoka kwa Watanzania waishio Uingereza kwenye mkutano uliofanyika kwenye Ubalozi wa Tanzania Jijini London, Uingereza.
Alisema watu watatu kati ya wanne nchini Tanzania wakiwemo watoto, wanamiliki simu za mkononi ambayo ni sawa na watu milioni 35 kati ya milioni 45.
Alisema sheria hiyo ilitugwa kwa misingi mitatu moja ikiwa ni kumpa mtumiaji uhuru wa kutoa maoni au taarifa, uhuru ambao alisema unalindwa kikatiba lakini akaonya kuwa kila uhuru unaotolewa pia una mipaka yake kama ilivyoainishwa kwenye ibara ya 30(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Alisema sheria hiyo pia inatoa uhuru wa mtu kuwa na faragha (privacy) na msingi wa tatu ni sheria hiyo kuzingatia matumizi ya mitandao ili kulinda usalama wa nchi.

No comments:

Post a Comment