umoja umataifa anaonya kuwa Burundi huenda
ikatumbukia tena kwenye vita, kama jumuiya ya kimataifa haitachukua
hatua za haraka kuzuia hilo.
Pablo de Greiff, mchunguzi maalum wa umoja mataifa kwa ukiukaji
mkubwa, anasema mengi yametokea tangu alipoitembelea Burundi mwezi
December, na hamna lilo zuri. Anasema ,Burundi imejiondoa kwenye njia
ya amani ambayo imeifuata tangu mwaka 2000, pale makubaliano ya Arusha
yalipomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.
Anasema serikali ya rais Pierre Nkuruzinza haijaribu tena kujenga
jamii kutokana na kanuni za sheria, na kwamba utamaduni wa kutokhifia
kushtakiwa kutoka miongo iliyopita umejikita zaidi na unatumiwa kama
nyenzo ya ukandamizaji na ghasia.
De Greiff anasema amewasilisha wasiwasi wake kwa baraza la haki za
binadam la umoja mataifa kwa matarajio nchi kuwa nchi wanachama
watafahamu ukubwa wa hali inayojitokeza nchini Burundi na kuchukuwa
hatua ili kuepuka janga kutokea.
De Grieff anasema, anataka kuwa muwazi, na kujaribu kutowa wito wa
haraka na wito wa tahadhari kwa jumuiya ya kimataifa, wasisubiri hadi
tufikwe na janga jingine mikononi mwetu kabla ya kuchukuwa hatua.
Takriban watu laki 3 waliuwawa wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Burundi.
Taifa hilo lilikuwa na Amani katika miaka ya karibuni hadi mwishoni
mwa mwezi Aprili, pale rais Nkuruzinza alipotangaza kuwania muhula wa
tatu madarakani. Tangu wakati huo, De Greiff anasema, kumekuwepo na
Zaidi ya mauwaji mia 1, mamia ya ukamataji holela na kesi nyingi za
mateso na kutendewa vibaya.
Anasema hamna kesi inayochunguzwa ila moja inayohusisha afisa wa serikali.
Rais alichaguliwa tena mwezi July, lakini mivutano bado ipo baina ya
wafuasi wake na wale wanaosema amekiuka katiba ambayo imeweka kiwango
cha mihula miwili tu kwa rais kuwepo madarakani.
Mchunguzi huyo wa umoja mataifa anasema jumuiya ya kimataifa na
serikali za kikanda haziwezi kumudu kukaa na kusubiri ukatili mpya
utokee tena nchini Burundi. Anaonya kuwa hii inahatarisha mzozo mkubwa
kuweza kutokea katika eneo la maziwa makuu, na matokeo ambayo
yanatisha na yasiyojulikana.
HABARI
ReplyDelete