Waziri wa Mambo ya N
je na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.
Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amewataka
wananchi kuwapima wanaotangaza nia ya kugombea nafasi za urais kama wana
maadili ya dhati katika kutokomeza rushwa.
Akizindua
Tamasha la Ulamaa la Qaswida katika shule ya Benjamen Mkapa jana, Membe
alisema uongozi wa heshima ni ule wenye kuzingatia maadili na
unaochukizwa na vitendo vya rushwa.
Alisema rushwa ni kero kubwa kwa wananchi, hivyo viongozi waadilifu pekee ndiyo wanaoweza kumaliza tatizo hilo.
“Wachujeni
viongozi wanaotangaza nia ya kuwaongoza, muwapime kama wana maadili ya
kutosha, wapimeni kama siyo wala rushwa,” alisema na kuongeza:(P.T)
“Rushwa
ni tatizo kubwa, viongozi wasio na maadili hawawezi kumaliza tatizo la
rushwa. Angalieni ni viongozi gani wenye sifa na maadili.”
Membe alisema watangaza nia hao wanapaswa kupimwa na wananchi hadi kwenye dini zao kama ni watu safi ambao wanafaa kuwaongoza.
Alisema
ni vyema wananchi wakatumia muda wa kuwapima viongozi hao katika mambo
mbalimbali na kuepuka kuwa wepesi wa kusikiliza kauli na kuzikubali.
“Uongozi
wa heshima ni ule wenye maadili. Viongozi bora ni wale watakaochukia
vitendo vya rushwa kwa nguvu zote, jamii imechoka kushuhudia vitendo
hivi vinavyonyima haki,” alisema waziri huyo wa Mambo ya Nje.
Katika
tamasha hilo, Membe aliahidi kuchangia kiasi cha fedha ambacho alikataa
kukitaja akisema yeye si mtu wa kutafuta umaarufu katika masuala kama
hayo.
“
Nitachangia katika tamasha hili, lakini sitasema hadharani ni kiasi gani
kwa sababu sitafuti umaarufu mwepesi kupitia hela,” alisema.
Kuhusu
ndoto yake ya urais, Membe alisema Juni 7, mwaka huu wananchi wakae
kwenye runinga zao kwani atatangaza nia ya kugombea urais na kuomba
ridhaa kwa CCM. Tayari makada wengine wa CCM wameshaweka hadharani
dhamira yao ya kuwania kiti cha urais katika Uchaguzi Mkuu baadaye mwaka
huu.
Tayari
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amezindua mbio hizo mwishoni mwa
wiki mjini Arusha na Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba alizindua
jana mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment