Meli ikiwa imebeba zaidi ya watu 450 imezama baada ya kukumbwa na upepo mkali katika Mto Yangtze kusini mwaChina.
Kwa
mujibu wa shirika la habari la serikali Xinhua watu wanane wameokolewa
mpaka sasa na kazi inaendelea ya kuwaokoa abiria wengine.
Waziri Mkuu Li Keqiang anaelekea katika eneo la tukio.
Meli hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka mashariki mwa mji wa Nanjing kwenda Chongqing kusini magharibi ilipozama.
Meli
hiyo, Dongfangzhixing - au Nyota ya Mashariki - ilikuwa imewabeba
abiria wa Kichina 405, wafanyakazi watano wa shirika la usafiri na
wafanyakazi 47 wa meli hiyo.
Nahodha
na mhandisi mkuu, ambao ni miongoni mwa waliokolewa wamekaririwa
wakisema kuwa meli ilikumbwa na kimbunga na kuzama haraka.
Kazi ya uokoaji imekwamishwa na upepo mkali na mvua kubwa. Meli hiyo ilizama katika kaunti ya Jianli katika jimbo la Hubei.
Kwa
mujibu wa shirika la utangazaji la serikali ya China, meli hiyo
inamilikiwa na Shirika la Meli la Chongqing Eastern ambalo linaendesha
shughuli za utalii katika maeneo matatu ya vivutio katika mto Yangtze.
Waliokuwa
katika meli hiyo wengi wao walikuwa watalii wenye umri kati ya miaka 50
na 80 wakiwa katika safari ya kitalii iliyokuwa imeandaliwa na kampuni
ya Shanghai.
Habari zinasema meli hiyo imepinduka.
Watu
ishirini na wawili waliufa katika mto huo mwezi Januari, wakati boti
iliyokuwa katika majaribio kuzama karibu na Zhangjiagang, katika jimbo
la Jiangsu.
No comments:
Post a Comment