Kibano! Mwendesha pikipiki almaarufu bodaboda aliyetajwa kwa
jina la Juma Abdallah amekula kibano baada ya kudaiwa kumdhalilisha
afande wa kike wa Jeshi la Zima Moto mkoani hapa, Winnifrida Kachota kwa
kumshika kalio hivyo kuibua timbwili zito.
Tukio hilo lililoibua vita kubwa lilijiri nje ya ofisi ya Zima Moto
mkoani hapa mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo ilibidi polisi wa Kikosi
cha Kutuliza Ghasia (FFU)…

cha Kutuliza Ghasia (FFU) kuingilia kati wakiwa na silaha nzito ambapo
walifyatua mabomu ya machozi ili kuwatawanya bodaboda hao waliokuwa
wakimtetea mwenzao.
Akizungumza na gazeti hili, bosi wa afande huyo, Mkaguzi Msaidizi wa
Kikosi cha Zima Moto na Uokoaji Kituo cha Morogoro, lssa lsandeka
alisema askari wake alidhalilishwa kwa kushikwa makalio wakati anakatiza
kwenye kijiwe cha bodaboda kuelekea kazini.
“Alipokuja kuripoti kwetu tulikwenda kuripoti tukio hilo na sisi
tulikwenda kumkamata bodaboda yule na kumpeleka polisi.“Cha ajabu, mmoja
wa bodaboda alisambaza ujumbe kwa bodaboda wenzake ambao walifika hapa
na kutufanyia fujo kubwa hivyo polisi wakafika na kutuliza ghasia.”
Katika tukio hilo, bodaboda hao walidaiwa kuwa walitaka kulipa kisasi
kwa maafande hao wa faya huku baadhi yao wakirusha mawe kwenye kituo
hicho.Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Mussa Mazambo
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba jeshi hilo linawashikilia
watuhumiwa 15 kwa uchunguz

No comments:
Post a Comment