Mwonekano
wa jengo la kushushia na kupandiashia abiria linaloendelea kujengwa
katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.
Uongozi wa Mamlaka za Viwanja vya Ndege
Tanzania wameshauriwa kuwa makini katika ujenzi unaoendelea wa jengo la
kutua na kupaa ndege katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius
Nyere (JNIA).
Ujenzi
huo unaotarajiwa kuongeza uwezo wa uwanja wa mara tatu zaidi umejikita
katika sehemu za maegesho ya magari, sehemu ya abiria kupumzika, sehemu
za abiria kupandia na kushuka kwenye ndege, ofisi za uhamiaji na huduma
zingine muhimu.
Mkurugenzi
mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Suleiman S. Suleiman amesema kiwanja cha
Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) hapo awali kilikuwa na uwezo wa
kuruhusu ndege sita tu kutua kwa saa lakini kwa sasa unaweza kuruhusu
ndege hadi 30. Tunatarajia kuongeza ndege zaidi na hivyo kuufanya
kiwanja hiki kuhimili 2500 tofauti na abira 700 wa awali pindi ujenzi
huu utakamilaka.
Kwa
sasa ujenzi umefikia asilimia 85, katika awamu ya kwanza ambayo
inategemewa kukamilika Juni mwaka 2016 na itakiwezesha JNIA kuhudumia
abiria milioni tatu na nusu kwa mwaka. Iwapo ujenzi wa awamu ya pili
utakamilika mwaka 2017 JNIA kitakuwa na uwezo wa kuhudumia jumla ya
abiria milioni sita kwa mwaka.
Alipokuwa
akitembelea mradi huo, Naibu Katibu Mtendaji- Ofisi ya Rais Tume ya
Mipango Bibi. Florance Mwanri, aliuambia uongozi wa Mamlaka hiyo
kuzingatia wazo la kuwa na huduma zote za msingi katika kiwanja cha
Julius Nyerere ili kuweza kushindana viwanja vya nchi jirani na barani
Afrika kwa ujumla.
“Ni
vema kuwa kiwanja chetu cha ndege kinapanuliwa ili kiweze kuhudumia watu
wengi zaidi, lakini nimegundua kuna vitu muhimu vimesahaulika katika
usanifu wa upanuzi huu, kuna vitu kama hoteli, jengo la hospitali,
sehemu za kupata huduma za kibenki na pia namna nzuri ya kuwapatia
abiria watuao usafiri wa kwenda mjini na sehemu nyinginezo, nadhani haya
pia yazingatiwe, alisema Bibi. Mwanri.
Uwepo
wa huduma hizi utawavutia abiria kutumia kiwanja chetu kuliko vya majira
zetu na pia kutakuza mapto ya TAA na taifa kwa ujumla.
Ujenzi
huu unaoendelea umezingatia haja ya kuunganisha majengo yote matatu ili
kurahisisha uunganishaji wa ndege za ndani na za nje pia upokeaji wa
mizigo.
Serikali
kupitia Tume ya Mipango, imeshaanza kuandaa Mpango wa Miaka Mitano
2016/17-2020/21 wenye dhima ya kukuza uchumi wa kiviwanda hivyo basi
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege inapaswa kuwa chachu ya mpango huu kwa
kusafirisha watu na bidhaa zitakazozalishwa na viwanda hivyo”alisema
Bibi. Mwanri.

No comments:
Post a Comment